Njia 3 za kuwa rafiki yako mwenyewe wa dhati

Sikiliza moyo wako na ujiheshimu.

Je, kuna wakati unahisi ni kama kuna watu wawili kichwani mwako? Je, kuna wakati unahisi ni kama wanabishana au hawapendani?

Tunaposaidia utu wetu kufanya kazi kwa pamoja, inaweza kutusaidia kuhisi wenye furaha na kuwa na ujasiri zaidi.

Hapa kuna njia tatu za kujaribu:

Tumia heshima.

Ikiwa wewe hukasirikia unapohisi umekosa, hauko peke yako. Lakini umewahi kugundua jinsi tunavyoweza kujizungumzia ndani ya vichwa vyetu kwa njia ambayo hatuwezi kumzungumzia mtu mwingine yeyote?

Kuwa mkali kunaweza kukufanya uhisi uko chini sana. Ungejibizana na mtu anayekuita majina au kusema wewe ni mjinga, sivyo? Kwa hiyo fanya hivyo wakati unapojikuta unafikiria mambo hayo kukuhusu pia.

Ukijikuta unafikiria kuhusu kitu kibaya ulichokifanya, fanya unavyoweza kumfanyia rafiki na ubadilishe mazungumzo kwa mambo yaliyofanyika vizuri. Jisamehe, tambua unachoweza kujifunza kutokana na kilichofanyika, na uhisi vizuri kwamba unakua.

Sikiliza.

Huenda umesikia kwamba kujisemesha ni ishara ya wazimu. Lakini inaonekana kwamba ni jambo zuri sana. Husaidia kupanga mawazo yetu, kupanga mapema na kujidhibiti.

Kwa hiyo jaribu kusikiliza sauti yako ya ndani na kuzungumza nayo! Unapoamka asubuhi, au kwenda kitandani usiku, sikiliza mawazo yako. Iwapo una hofu inayokusumbua usiitupilie mbali. Sisi sote tuna hofu. Ikiwa rafiki angetujia akiwa na wasiwasi tunaweza kuuliza: ni kwanini una hofu, unaogopa nini kitafanyika? Kuna hatari yoyote ya kweli? Ikiwa kuna hatari ya kweli tutasema jiamini. Kama sivyo, tutasema kuwa jasiri na ushinde hofu yako. Tunapaswa kuwa wakarimu kwetu pia kama tunavyowafanyia marafiki zetu. Ikiwa tunaamini wana uwezo wa kushinda hofu yao, kwa nini tusiweze kushughulikia vyetu wenyewe?

Tumia ushauri wako mwenyewe

Fikiria kuhusu ushauri unaoweza kumpa mtu. Uandike chini, subiri dakika chache, kisha usome. Kwa kweli unaweza kusema unafuata ushauri huo wewe mwenyewe?

Kwa kawaida hisi rahisi zaidi kutoa ushauri badala ya kuutumia. Na wakati tunahisi tunahitaji ushauri mzuri sisi wenyewe, mara kwa mara sisi huhimizwa na yale wanayofanya watu wengine kuliko wanachosema.

Jaribu kuishi kulingana na ushauri wako mwenyewe na utawahimiza wengine zaidi ya maneno yako ya busara. Ni vizuri kuwahimiza wengine, kwa kuwa hutufanya tuwe na furaha zaidi na kuweza kujiamini zaidi.

Share your feedback