Kwa KILA msichana
Ninajihisi mrembo ninapojiamini, ninapokuwa mwenye nguvu na ninapoweza kukabiliana na lolote. Nilivyokuwa kinakua, mwili wangu ulipitia mabadiliko mengi ya kihisia na ya kimwili, ilikuwa rahisi kusahau urembo wangu.
Lakini niliweza kupata njia ya urembo halisi na niko tayari kushiriki siri zote pamoja nawe. Siri kubwa ni ipi? Tayari una mambo yote unayohitaji!
Kubali tofauti zako
Nilikuwa naona aibu juu ya madoa niliyokuwa nayo usoni, kwani hakuna rafiki yangu aliyekuwa nayo.. Kila nilipozidi kukua, niligundua kwamba maumbile ya kipekee ya kila mtu ndiyo yanayowafanya kuwa warembo.
Siwezi kubadilisha ninavyoonekana – siwezi kujirefusha au kubadilisha rangi ya macho yangu. Lakini siyo lazima. Kila mtu ni tofauti na utofauti ni urembo!
Wewe pekee ndiwe unayeweza kufafanua urembo
Majarida na mtandao unaonyesha wazo dogo kuhusu urembo. Badala ya kuangalia pale, angalia vile vinavyokuzunguka ili uone urembo halisi. Angalia kwenye kioo au watu karibu nawe. Siyo ngozi kamili au meno yanayowafanya watu kuwa warembo – kinacho watofautisha watu ni jinsi walivyo wacheshi au jinsi walivyo marafiki wazuri!
Uliza watu wengine
Ni rahisi sana kusahau mambo yanayotufanya kuwa warembo. Wakati mwingine – unahitajika kumwambia mtu mwingine akukumbushe. Niliwauliza marafiki zangu ni kitu gani kirembo kwangu na wakasema, tabasamu langu la mzaha, jinsi kicheko changu kilivyo kikubwa na jinsi ninavyo wakumbatia kwa uchangamfu.
Jipende kwanza
Mafuta mapya ya kujipaka uso au kujipodoa siyo siri ya urembo. Urembo halisi unaanza kwa kuupenda mwili wako. Kama tu kinachohitajika kwa maua ili yastawi – mwili wako unahitaji kiwango sahihi cha maji, jua na virutubishi. Kula kinachokufanya uhisi vyema na kunywa maji ya kutosha – utang’aa!
Toa jasho
Ninajihisi mrembo zaidi baada ya kukimbia – hata kama uso wangu umekuwa mwekundu na nimefunikwa na jasho. Ninajihisi kuwa mwenye nguvu na mzima wa afya. Kufanya mazoezi huujaza mwili wako na homoni za furaha na inakusaidia kujihisi mrembo kwa ndani na pia bora zaidi nje. Tafuta mchezo au zoezi linalokufanya ujihisi mwenye nguvu!
Share your feedback