Ni wakati wa kujichunguza
Siku nyingine unaweza kujisikia vizuri sana, na siku nyingine hutaki kutoka nyumbani au kuonyesha uso wako kwa mtu yeyote. Ni vigumu kujaribu kila wakati kuwa sawa na kile ambacho kila mtu anasema ni kizuri na kinafaa.
Jambo muhimu kuhusu kujiamini na kuwa na furaha kivyako ni kuepuka kuingia katika mtego wa kuamini visasili hivi vitano!
Ukweli: Unachoona katika sherehe, shule au kazini, na hasa katika mitandao ya kijamii, huwa si kweli kabisa. Inapofikia wakati wa kujisikia vizuri, jambo muhimu zaidi ni kwamba sisi sote hupata chunusi, sisi sote tuna kasoro, na wakati mwingine sisi sote hujishuku. Cha maana, ni kwamba unajipenda mwenyewe, matatizo yako na kila kitu! Jaribu kuimarisha imani hiyo kwa kurudia kitu kimoja unachopenda kila asubuhi.
Ukweli: inafurahisha sana kujaribu vipodozi tofauti. Lakini hisia hizi ni za muda tu. Wewe pia ni mrembo unapokuwa hujajipodoa na wakati umevaa tisheti na mitindo yako ya zamani uipendayo. Kumbuka, kuwa mrembo ndani ndiyo muhimu. Kubalianeni na marafiki zako mjaribu kukaa siku moja kwa wiki bila kujipodoa!
Ukweli: Ingekuwa watu hawahuzuniki, wangekuwa roboti! Ni kawaida kabisa kuwa na hisia tofauti. Ikiwa wewe ni mwaminifu na marafiki zako kuhusu unavyojisikia wakati mwingine, wanaweza pia kufunguka kwako pia. Hii itawasaidia kama kikundi kuhimizana na kusaidiana na kukuza imani.
Ukweli: Wakati una mtu anayekiri mapenzi yake ya dhati kwako kila wakati, kwa hakika hukufanya ujiamini! Lakini kuwa mwanamke anayejiamini na mwenye furaha huanza na wewe.
Ukweli: Wakati mwingine unahisi ni kama hakuna mtu anayekusikiliza, au kukuelewa, na wanakuchekelea tu, hata wakati unasema ukweli. Ikiwa unahisi haueleweki, jaribu kuchukua hatua mbili nyuma na uangalie hali yako kutoka kwenye mtazamo tofauti. Pengine kuzungumza na watu hao kwamba unahisi hawakuelewi kunaweza kusaidia ueleweke zaidi na kukupa ujasiri wa kukufanya uongee wakati una jambo muhimu la kusema.
kwa hiyo wakati mwingine unahisi umenaswa na visasili hivi, jiangalie kwenye kioo na ujiambie: "Mimi ni mrembo, nina nguvu, ninaweza!
Share your feedback