Sababu 5 kwanini wewe ni wa pekee sana!

Fikia ndoto zako kwa kuwa na mtazamo unaofaa!

Kuna wakati unahisi kama huwezi kufikia ndoto zako?

Niko hapa kukujulisha kitu – unaweza kufikia ndoto zako. Kujiamini ni hatua ya kwanza katika safari ya kufikia ndoto zako.

Kujiamini ni muhimu sana. Hutusaidia kuwa na mtazamo unaofaa katika kufanikisha malengo yetu. Ujasiri hutusukuma kusonga mbele wakati tunapitia magumu katika maisha, hata ule wakati tunahisi kukata tamaa. Tunapokosa ujasiri mambo huonekana kuwa magumu na hata hutufanya tujihisi kupungukiwa au hata kukosa motisha kabisa.

Kuna mambo mengi unaweza kufanya kujenga ujasiri wako… kwa mfano, kusoma stori za watu mbalimbali, Lakini njia bora hasa ya kujenga ujasiri wako ni wewe binafsi kujiamini mwenyewe!

Hio ni kweli kabisa! U wa pekee sana kwa jinsi ulivyo.

Hizi hapa sababu tano za kwanini tunasema u wa pekee:

  1. Wewe ni Mpambanaji! Kutaka kujenga ujasiri wako tayari kunaonyesha kuwa wewe ni mfanya maamuzi mwenye malengo na oliyekusudia.
  2. Una uwezo! Unaweza kushindwa kumbeba tembo kwa mkono mmoja lakini umeweza kukabiliana hali ngumu katika maisha
  3. Wewe ni mjanja! Kumbuka zile nyakati ambazo oliweza kufanya jambo peke yako! Lazima olitumia akili sana kufanya hivo.
  4. Wewe ni mkarimu! Una roho nzuri kwa wengine.
  5. Wewe ni jasiri! Hofu au wasiwasi hutokana na msukumo wa kutaka kufanya vizuri katika kitu folani, na si mbaya. Kujiamini haimanishi huna wasiwasi tena, inamaanisha kwamba unaweza kufanya jambo hadi kufikia lengo lako ndani ya hofu yako.

Kamwe usichukulie poa uwezo ulionao. Kujitathimini ndani ni njia nzuri ya kugundua ukweli juu ya uwezo ulionao

Hapa kuna haka ka zoezi: Andika angalau mambo 3 unayopenda kuhusu tabia yako; labda ni mwenye ndoto kubwa, huwa unachekesha wengine au wewe ni mkarimu.

Kisha, kila wiki, ongeza kitu kimoja tena Ukiweza, endelea kuongezea kwenye orodha halafu unaweza kuipitia unapojisikia u mnyonge.

Kamwe usiache kujikubali dada! usipojikubali nani atakukubali?

Share your feedback