Hatua 5 za kutumia kujieleza

Ni rahisi mno

Unakumbuka ule wakati uliokuwa unahisi kama hakuna anayekusikiliza?

Pengine ulikuwa na rafiki aliyekuwa akipinga ile mipango yako ya baada ya kumaliza chuo. Au pengine wazazi walitaka uwe daktari na sio meneja. Maamuzi haya ni ya muhimu sana na inaweza kukufanya uhisi kukerwa na kuonewa. Au sio?

NI muhimu kujieleza na kuhakikisha wengine wanakusikiliza. Labda hujui namna ya kufanya hivi.

Hapa kuna vidokezo 5 vya kukusaidia!

  1. Amini hisia zako za ndani – kama kuna mtu amesema ama kufanya jambo na unahisi hajafanya poa,basi kuna uwezekano haliko sawa sawa vilevile. Amini kwamba wewe binafsi unaujua uonevu wa aina yoyote pale unapouona.
  2. Jiamini lakini pia heshimu wengine – Unapojieleza, ongea polepole na kwa utolivu. Unaweza toka kwa muda kidogo unapohisi hasira imepanda. Hii itakusaidia utolie ili uongee mambo ya maana.
  3. Kumbuka kumsikiliza unaeongea naye – anaweza kuwa ni mtu ambaye hakubaliani na wewe kimtazamo, lakini pia yeye anastahili kusikilizwa. Ukifanya hili utaanza kuelewa kuwa tumeumbwa tofauti hata kwenye kufikiri pia . Kuna wakati unaweza kutokubaliana kuhusu chuo kipi uende au kampuni gani ukafanyie kazi. Hilo ni , jambo la kawaida kabisa.
  4. Hakikisha unachangia kwenye mazungumzo kutokana na jinsi uonavyo wewe binafsi– Tumia “mimi” unapoanza kuongea. Mfano kwa kusema kama hivi “Mimi naona haikua vizuri kunikatisha nilipokuwa naongea.” kuongea hivyo ni bora koliko kusema “Una tatizo gani wewe? Usinikatishe ninapokuwa naongea ”. Kumbuka watu hujibu vizuri zaidi wanapohisi hawalengwi wao.
  5. Kuwa muwazi kuongea kuhusu mambo unayotamani kuona yakifanyika na uelezee kwa utolivu.Kwa mfano, pengine ungetaka wazazi wakubaliane na chaguo lako la chuo. Waeleze kwa njia nzuri na ya adabu.

Share your feedback