Hivi ndivyo urafiki wa dhati unavyoweza kuboresha maisha yako.
Marafiki wazuri wanaokuunga mkono ni wale wanaotuhimiza kufanya kazi kwa bidii, wanaotukumbatia na kutoa ushauri wakati tunapojisikia vibaya na kwa ujumla hufanya maisha yetu kuwa bora zaidi.
Hapa kuna hali 5 ambazo unaweza kuzishinda kwa urahisi ukiwa na rafiki mzuri kando yako.
Kuachana na mpenzi wako huwa ni wakati mgumu na unaochanganya kwa wengi wetu. Lakini kuwa na marafiki unaowaamini wa kuwategemea huifanya iwe rahisi unapopitia maumivu haya ya moyo.
Kuongea na mtu au wasichana wako marafiki kuhusu maumivu unayohisi kunaweza kukupa ahueni au kukuchangamsha. Kuwa pamoja na marafiki zako kunaweza pia kuwa njia nzuri ya kutoa mawazo kuhusu mpenzi uliyempoteza.
Kwanini usumbuke na kazi ya shuleni wakati una marafiki?
Kwa hiyo wakati mwingine una matatizo ya kutatua hesabu au kuandika kitabu hicho katika somo la Kiingereza, omba msaada kutoka kwa marafiki zako ambao wanafahamu vyema zaidi masomo hayo kuliko wewe.
Wakati mwingine dhalimu atamnyanyasa mtu ambaye anaonekana yuko peke yake na hana mtu wa kumtetea.
Lakini unapokuwa marafiki wanaokuunga mkono ambao unaweza kuwa nao wakati wa chakula cha mchana au kutembea nao baada ya shule, wanakuwa kinga ya ulinzi dhidi ya udhalimu.
Ikiwa tayari umedhulumiwa usifikirie kama jambo la aibu au la kudhalilisha. Shida ni anayekudhalimu wala si wewe, kwa hiyo ongea na marafiki zako wa karibu na kwa pamoja mnaweza kupata njia za kuripoti udhalimu huo kwa wazazi au shule yako.
Kuzungumzia kuhusu matatizo uliyonayo nyumbani kwa rafiki wa kweli kunaweza kukupa faraja na matumaini. Kuwa pamoja na rafiki yako kunaweza pia kuwa njia nzuri ya kusahau matatizo ya nyumbani ambayo huwezi kuyadhibiti.
Kuchukua muda kumwelezea rafiki unayemwamini ni njia ya hakika ya kuimarisha urafiki na kutengeneza urafiki wa maisha.
Pengine unafikiria wewe si mwerevu vya kutosha, au kwamba wewe ni mkubwa sana au mdogo sana - kuwa na marafiki wazuri kunaweza kukusaidia kuongeza kujiamini. Marafiki wa kweli hukuhimiza kuona urembo wako wa ndani badala ya kulenga dosari zako.
Kumbuka, rafiki wa kweli yuko hapo kuboresha maisha yako kwa kukuunga mkono, kukujali na kuwa mwaminifu.
Share your feedback