Sauti Yako ni ya Muhimu
Hebu fikiri mtu mwingine anakuamulia nini kinafaa kuvaa, muziki gani unapaswa kusikiliza na hata unapaswa kujifunza masomo gani chuo kikuu. Kwa bahati mbaya, hii inatokea kwa wasichana wengi duniani, ambao wanafikiri maoni yao siyo muhimu isipokuwa kwa wao wenyewe, na hivyo hawaongei. Ukweli wasichana wengi wanashindwa kuongea sababu wanaambiwa na familia na rafiki zao, kuwa wanatakiwa kuwa kimya, wapole na watulivu. Na mimi niko hapa kukukwambia kuwa unaweza kuwa mpole na mtulivu lakini pia ukaongea maoni yako. Kiuhalisia wasichana wengi wana ujuzi unaowawezesha kuongea na na umma, wanachohitaji ni kutiwa moyo.
Kwanza kabisa, wasichana wana maoni!
Wakati wasichana wengi wanaongea sana wakiwa wenyewe, wanapata changamoto kuongea mbele ya umma. Mara nyingi wasichana wanaogopa kuongea mawazo yao hadharani sababu wanaogopa kuchekwa. Lakini ni muhimu kuwapa watu mtazamo tofauti; unajuaje, labda utabadilisha mtazamo wa mtu. Cha msingi ni kujua utaongea nini na kwanini unaongea hilo jambo.
Igiza mpaka uweze
Kuongea hadharani kunahitaji kujiamini, lakini sio rahisi kujiamini mara moja. Unaweza kujifanya unajiamini hata kama siyo hivyo. Hamna anayeweza kusoma akili yako, hivyo hamna atakayejua, wakatacho ona ni mtu ambaye yuko tayari kutoa maoni yake.
Kujaribu kuna boresha
Unavyofanya kitu mara nyingi ndivyo kinakuwa bora zaidi. Hivyo usikate tamaa ikiwa unaogopa au kusahau kile ulichotaka kuongea. Itakuwa rahisi baada ya muda. Kumbuka kuna mambo mengi ambayo wasichana hufanya kila siku, ilikuonyesha uwezo wao. Hivyo japo kuongea kwa umma kunaweza kuwa kugumu, unao uwezo wa kujaribu na kuweza.
Share your feedback