Je umezungukwa na marafiki wabaya?

Jifunze kutengeneza marafiki wazuri katika maisha

Mambo vipi msichana!

Je unadhani hivi sasa umezungukwa na watu wabaya, unaambatana na watu ambao sio marafiki zako haswa?

Unapotumia muda mwingi ukiwa umezungukwa na watu wabaya huathiri maisha yako. Hivyo ni vyema kuzungukwa na watu wenye mtazamo sahihi watakao kuruhusu kuishi kama ulivyo na watakutia moyo na kukuunga mkono.

Sasa Je unawezaje kuondoka katika makundi ya watu wabaya na kujiunga na watu wema? Zifuatazo ni dondoo zinazoweza kukusaidia.

  • Tambua makundi ya watu wabaya yalivyo. Kama unazungukwa na watu wanaokucheka, wanaokushusha na kukufanya ujisikie vibaya hii inamaanisha umezungukwa na watu wabaya.

  • Tafuta kundi la marafiki ambao watakuwa na uwezo wa kukusamehe na kukukubali jinsi ulivyo. Hakuna aliyekamilika na wakati mwingine unaweza kumuumiza rafiki yako au hata kuvunja uaminifu kwake. Rafiki wa kweli husamehe na huwa tayari kuendelea na maisha.

  • Tambua sifa za marafiki wazuri. Marafiki wazuri ni watu ambao hukupenda na kukuamini na kukuunga mkono katika kila hatua unayoipitia. Lakini pia watakusaidia kufanya maamuzi sahihi na hawatokusukuma kufanya vitu ambavyo haupo tayari kuvifanya.

  • Jifunze kutafuta watu ambao hupendelea kufanya mambo mazuri unayoyapenda. Chagua marafiki wenye ndoto za kuendelea na shule, wanaotamani kufanya vizuri shuleni, na wenye kujitengenezea fursa katika maisha yao. Huwa wananafasi nzuri ya kufanikiwa kama itakavyokuwa kwako.

Huwa sio kazi rahisi kutengeneza marafiki wapya lakini kama utakuwa mkweli na muwazi utapata watu sahihi. Urafiki mzuri huja bila kulazimisha hivyo usihofu jinsi watu wanavyokuchukulia. Jitahidi kuwa mtu mwema na hakika watu sahihi watakuja katika maisha yako.

Share your feedback