Maisha ya Mjini

Jinsi nilivyoshinda

Jina langu ni Aisha na nina miaka 15,Nilikuwa naishi kijijini mpaka pale Baba yangu alipopata kazi,tukahamia mjini,kwa upande mmoja nilikuwa nasikia huzuni kuwaacha marafiki zangu na mwingine nilikuwa na shauku ya kupitia maisha mapya.

Kutembea gizani

Nilijisikia Kusisimka wakati napita getini kwenye shule yangu mpya. Nilikuwa nimetoka darasa la watu 10 hadi 50! Hakuna aliyenifahamisha kwamba watoto wa huonekana tofauti hata mavazi yao pia, Baada ya shule nilikuwa nikiona kila mtu akibadilisha nguo na kutupia Jinsi na raba,wakati mimi nipo na sendoz na sketi yangu ndefu.

Changamoto kuhusu Asili yangu

Ilikuwa dhahiri kwa wanafunzi wenzangu kwamba sikuwa natokea eneo hili. Matamshi yangu yalikuwa kitofauti na mavazi yangu vilevile, hivyo watu walinidharau kwa sababu hawakunielewa. Nilipata presha ya kutaka kufanana naoWalimwengu hushangaza sana wakati mwingine,Wanakwambia kuwa wewe lakini wakati huo huo wanataka ufanane nao.Wanakwambia Wanakwambia jiachie kuwa huru lakini lazima iwe sawa na matakwa yao. Inachanganya sana"

Mama Msaada wangu

Mama yangu aliweza kugundua kuwa nashindwa kuendana na haya maisha ya mjini kwa hiyo akanipa siri kubwa sana,Aliniambia kwamba siku zote watu hutaka tuwe watakavyo wao na hata muonekano pia, kumbe hivyo vitu si vya muhimu hata kidogo maishani.Cha muhimu ni kuwa na roho nzuri, kujiamini binafsi na uwezo ulio ndani yangu.Si ni kweli?

Kujiamini wakati wote

Siku iliyofuata nilienda shuleni nikiwa mchangamfu. Sikubadili nguo zangu wala kuongea kwangu Wakati watu walipokuwa wananicheka nilikuwa natabasamu tu kwa sababu nilitambua kuwa mimi ni wa thamani siku zote. Mimi ni mwerevu na na mwenye nguvu na hilo ndilo la msingi. Mazingira mapya yanaweza kuwa changamoto, lakini kamwe usijisikie aibu kuhusu jinsi ulivyo. Jiamini wakati wote kwasababu duniani kote hakuna mwingine kama wewe,Ni wewe peke yako na hicho ni kitu cha kipekee!

Share your feedback