Je una Changamoto za boifrendi?

Hii ndio njia ya kuliongelea hilo.

Mawazo yako (6)

Hebu piga picha ya tukio kama hili:

Umekuwa ukivutiwa na mvulana mmoja kwa muda sasa. Na mkaanza kupiga stori na baadaye akakuomba uwe mpenzi wake.Anatamani kuyapeleka mahusiano yenu katika hatua kubwa zaidi.

Unaamua kumkubalia ombi lake kwani kila kitu kinaonekana kipo sawa, lakini ukweli ni kwamba hata hauelewi nini unafanya.

Mara ghafla mpenzi wako anataka muanze kuwa mnaonana sehemu ambazo mtakuwa peke yenu tu au masaa ya usiku anataka uende chumbani kwake.

Hujisikii vizuri kufanya hivi.Haupo tayari kufanya ngono ila inaonekana wazi hili ndilo jambo tu analolitaka.

Sasa unataka umchane vile unavyojisikia halafu ndipo uweze kufanya maamuzi kama upo tayari kuendelea na mahusiano haya au laa!

Unaona kama haya maamuzi ni makubwa sana, ambayo huwezi kuyafanya mwenyewe. Sasa je ni nani unayeweza kuzungumza naye kuhusu jambo nyeti kama hili na unaanzaje kumueleza?

Basi huu hapa ushauri kutoka kwa dada zako wakubwa.

1. Chagua mtu sahihi

Unahitaji kumpata mtu ambaye utajisikia huru ukiwa naye na ambaye unaweza kumuamini na atakuwa mkweli kwako Hakikisha yoyote utakayemchagua kuzungumza naye awe na vitu hivi:

  • Mwaminifu
  • Mwenye uzoefu
  • Asiyeweza kukuhukumu

Unatakiwa kumchagua mtu ambaye atakuelewa na hatokuwa mwepesi kukuhukumu. Hupaswi kutafuta mtu atakaye kufanya ujisikie kuaibika au hatia hasa pale ambapo hujafanya kitu chochote kibaya.

2. Ni muda wa kufunguka

Kama kuna kitu chochote kinakusumbua, unapokizungumza inakusaidia kuzielewa hisia zako. Unapotaka kufunguka inakupasa uwe jasiri ila itakusaidia kujisikia vizuri hasa kama utazungumza na mtu sahihi. Angalia dondoo hizi hapa chini.

  • Usijikie aibu ama kuogopa kuzungumza kuhusu wavulana. Kumbuka kuwa mama, shangazi na ndugu zetu wengine wakubwa wamepitia mambo kama haya haya unayoyapitia hivi sasa. Wanaelewa hivyo, tulia na uwe jasiri.
  • Unapotaka kufanya mazungumzo tafuta eneo ambalo ni tulivu ili kusiwe na kelele na hakikisha yule unayeongea naye ni mchangamfu na hana msongo wa mawazo.
  • Fanyia mazoezi ya kile utakachokwenda kukizungumza. Kama unahofia kwamba unaweza kupaniki au kutetemeka basi kufanya mazoezi ya kile utakachokisema ni jambo la muhimu na unaweza kufanya hivi ukiwa umesimama mbele ya kioo. Kitu kingine kinachoweza kuwa msaada ni kuandika pointi zako.

Maisha huwa magumu mno hasa pale unapotaka kuishi ya peke yako bila kuomba msaada. Kama unahitaji ushauri wa namna ya kufanya maamuzi hasa ya mambo makubwa kama haya usiogope kuomba msaada.

Share your feedback

Mawazo yako

kwl maon yang kilich adikwa nisaii cn 2 me nampongez cn na cn ,

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Asante sana Nicodemus kwa kutupa mrejesho. Tafadhali washirikishe na rafiki zako ujumbe huu. Asante.

nimeweza kujifuza vitu vingi katika maisha hv asanten kwa kunisaidia mawazo

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Asante sana kwa kutupa mrejesho. Tafadhali washirikishe na rafiki zako ujumbe huu. Asante.

na pia ni vizuri sana kumpata unae muamini

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Upendo ni kivuli ukipata akupendae

Machi 20, 2022, 8:25 p.m