Kujitambua

Namna ya kujitambua "Wewe" ni nani.

Je hii imeshawahi kukutokea? Ile Siku, tu ndio umeamka, Mara paa! unajiangalia kwenye kioo, He? “MUNGU WANGU! HUYO KWENYE KIOO NI MIMI! AU MTU MWINGINE?”

Wote tumewahi kupitia nyakati kama hizo haswaa wakati wa ujana,mambo yanapokuwa yamebadilika, Kwa hiyo wewe ni nani ?haswa,yaani Yule mtu alie ndani yako ni “nani”, na Yule mtu ndani yako ambae huwa unaji igizisha tu ni nani? Kuyatafakari yote haya inaweza kuonekana kama inaogopesha,lakini wala usijali, ni safari tu ya kujifunza mambo mapya.

Jitengeneze
Unaweza kuwa yeyote unayetaka kuwa! Ni mambo gani ambayo yanakufanya kuwa mwenye furaha zaidi? Vipaji vyako ni vipi? Ni nini unachoweza kufanya vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote? Je, wewe ni mkimbiaji mwenye kasi zaidi darasani kwako? Mpishi mahiri kwenye familia yako? Msichana mchangamfu zaidi mtaani? Angalia kile unachoweza kufanya vizuri zaidi, na unachokipenda, kisha ujinoe zaidi— huenda ukagundua mambo mawili matatu kuhusu wewe.

Dora, ni mwanafunzi wa shule ya sekondari mwenye umri wa miaka 15, alituambia kuwa kwa kutambua kwamba alikuwa na kipaji cha sanaa ya uchoraji ,na ilimfanya awe mbunifu zaidi. Aligundua kwamba angeweza kujieleza na kuelewa hisia zake vyema zaidi kupitia michoro zaidi kuliko maneno. Alitumia sanaa yake ya uchoraji kuwachekesha marafiki zake, kuonyesha upendo kwa familia yake, na kuzielewa hisia zake — ziwe za furaha au za huzuni!

Haya safari inaanza sasa Woyoooo!
Je bado huna uhakika wa kile unachoweza kufanya vizuri zaidi? Usijali! Njia pekee ya kujua hili ni kujaribu vitu vingi tofauti kadri utakavyoweza. Kila siku Jaribu kufanya kitu kipya, hata kama kinaonekana kidogo au cha kijinga— na hata kama unahisi kama hautokipenda.

Lea, ni mwanafunzi wa chuoni mwenye umri wa miaka 20, alituambia kama isingekuwa ile twisheni ya kiingereza alioipata akiwa shule ya msingi basi leo hii asingeweza kusoma hii kozi ya Lugha. Mwanzoni hakuwa anapenda hata kidogo mambo ya Lugha, lakini mabesti zake walikuwa wanasomea hiyo kozi na yeye akaona ajiunge nao pia ili wapate muda mwingi wa kuwa pamoja! Hakuwahi kuwaza kama hili lingekuja kutokea lakini baadae alijikuta anapenda kujifunza lugha na sasa hivi ndio imeshakuwa taaluma yake.

Jiamini
Haijalishi ni nini unachokigundua kuhusu wewe, vitu unavyopenda au vipaji vyako, Kumbuka kuwa wewe utabaki kuwa ‘wewe’, na WEWE NI WA PEKEE. Hata kama maisha yanaonekana kuwa magumu na yenye changamoto, unapaswa kujiamini. Usiogope kuwa “wewe” popote ulipo. Kila uzoefu tunaoupata huwa ni fursa nyingine ya kujifunza na, kufanya makosa ni sawa tu na stori ya kuchekesha utakayokuja kuwasimulia marafiki zako.Jiamini, kwa sababu sisi tunakuamini!

Share your feedback