Kugundua vipaji nilivyo navyo

Ni Jinsi Gani Kusaidia Wengine,Kulifanya Nijiamini Zaidi

Habari! Jina langu ni Sophia, nina umri wa miaka 14 na ninaishi na mama na bibi yangu.Mtaa tunaoishi huwa ni mtulivu sana,huwa hauna makelele. Kwa bahati mbaya, siku moja usiku kitu kimoja cha ajabu kilitokea.Vyumba vya madarasa mawili ambavyo ni vya darasa la nne la tano vya shule ya msingi iliyopo mtaani kwetu viliungua lakini kwa bahati nzuri hakukuwa na majeruhi hata mmoja.Hivyo iliwalazimu wanafunzi wa madarasa hayo kusomea nje.

Kila jumapili huwa naenda kumtembelea bibi yangu.Ingawa sipendelei sana kutoka nyumbani,lakini kumtembelea bibi inanifanya angalau niwe bize, hasa kipindi cha likizo.

Siku moja jirani yake bibi alitueleza kuwa kuna kampuni ya ujenzi ilisikia habari juu ya madarasa yaliyoungua kupitia radio na kuamua kuchangia vifaa vya ujenzi ili madarasa hayo yajengwe upya.Hivyo walihitajika watu wa kujitolea kusaidia katika ujenzi.

Niliwaonea huruma sana wale wanafunzi,hivyo nikatamani kusaidia kwenye ujenzi,ingawa kiukweli nilikuwa naogopa mno maana sina ujuzi wa kitu chochote hata wa ujenzi pia,Niliamua kujitolea hivyohivyo kwa sababu nilikuwa bado nina muda wa kutosha.

Waliniweka kwenye timu ya usimamizi,na kazi yetu kubwa ilikuwa kuhakikisha hakuna matumizi mabaya ya vifaa vya ujenzi maana tungepata shida kama simenti ingeisha kabla ya kumaliza ujenzi wa madarasa! Kila siku ilinibidi niwe narekodi vifaa nilivyokuwa nikivitoa kwa wafanyakazi,na vile vinavyobakia. Lilikua jukumu zito mno,na mwanzoni nilihisi nakosea.Lakini niliamua kutulia, na kupiga kazii zaidi na kadri siku zilivyozidi kwenda nikawa mtaalam zaidi.

Ilituchukua muda wa wiki nne ili kukamilisha ujenzi! Na mwisho nilijivunia sana kuwa sehemu ya timu hii.. Hii ikanifanya niwaze jinsi ambavyo siku zote nimekuwa mtaalam katika kuandika mipango,Kwa mfano,siku zote mama yangu hunipa kazi ya kuandika ratiba ya vyakula vitakavyopikwa wakati wa sikukuu.

Kusaidia watu wengine kumenifanya niweze kutambua kipaji nilichonacho na kwamba kumbe naweza kuwa ni mtaalam wa kufanya kitu flani pasipo mimi kujua.Kwa nini na wewe usijaribu kutafuta kujua kipaji chako?.Huenda kujitolea kufanya kazi flani kutakusaidia kukigundua.

Jamani, baada ya mimi kugundua kipaji changu l pia kusaidia watu wengine,imenifanya nijifunzqe mengi,kwanza kabisa nimegundua Mimi ni wa muhimu sana,pia napaswa kujiamini kwa uwezo wangu nilionao.Kubwa zaidi ya yote imeniongezea ujasiri wa kujaribu mambo mengi mapya!

Share your feedback