Namna ya kufanya unachokipenda. ukisaidiwa na wazazi wako!

Tumia maneno haya 3 "Ameizing"/ya ukweli

Wande alikuwa na umri wa miaka 14 alipoanza kupenda muziki. Siku moja alipokuwa akielekea nyumbani kutoka shuleni alisikia muziki mzuri wa kuvutia kutoka kwenye jengo flani hivi lililokuwa mbali. Aliifuata sauti iliyomwelekeza kupita kwenye ki njia kinachoelekea kwenye hilo jengo. Alipigwa na bumbuazi hakuamini alichokiona.Ni kundi la vijana kama yeye wakiimba na kucheza vyombo mbalimbali vya muziki.

Wande alikuwa akichungulia huwa akiwa amejibanza kwenye kona ili asionekane. Alitambua kuwa kiongozi wao alikuwa ni Kabogo ,mwalimu wake wa sayansi shuleni kwake. Aisee inashangaza sana. Mwalimu Kabogo na Muziki wapi na wapi? Ghafla simu yake ikaanza kuita. Kumbe Mamayake alikuwa anapiga simu. Kelele ya sauti ilimfanya wamuone, aliruka chap na kukimbia..

Siku iliyofuata darasani kwenye kipindi cha sayansi mwalimu wake,Kabogo , akamwuliza, "Je, yule alikuwa ni wewe, Wande, nilikuona ukichungulia kwenye darasa langu la muziki jana” Wande kwa aibu aliitikia kwa kichwa.

"Ungependa kujifunza kucheza chombo cha muziki?" Aliuliza Bw. Kabogo.

Wande alikuwa anatambua jinsi gani alikuwa anapenda Muziki. Alitamani kuona muziki utampeleka wapi.kwa hiyo ndiyo. Hata akakubali ,ila kimbembe kinachobaki ni kuwashawishi wazazi wake.

"Sidhani kama wazazi wangu wataniruhusu," Wande aliongea kwa sauti ya chini.

Kisha Bw. Kabogo n alimpa Wande ushauri wa jinsi ya kupata sapoti ya wazazi au walezi wako

1. Kujitolea

Unapokuwa mdogo ni rahisi kupoteza uelekeo. Kila kitu huonekana cha kufurahisha na cha kusisimua, lakini huwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja. Ikiwa wazazi wako watawekeza fedha katika masomo ya muziki wanahitaji kuhakikishiwa kuwa utaendelea na hautakata tamaa au kuboreka kirahisi na kuacha.Hivyo mara zote wakumbushe nyakati ambazo uliwahi kukamia kulifanya jambo na likatokea.

2. Shauku, shauku na shauku zaidi

Waonyeshe wazazi wako jinsi ulivyo na shauku ya kujifunza chombo cha muziki. Zungumza nao kuhusu jinsi unavyopenda muziki. Zungumza nao kuhusu jinsi muziki unavyokusisimua na kuwashawishi kuwa una uwezo wa kuwa mwanamuziki bora.

3. Waelezee maono yako

Unatarajia kunufaika vipi kutokana na kujifunza chombo kipya? Waeleze! Waonyeshe ujuzi wote mpya utakaojifunza na fursa zote mpya ambazo zitatokana na muziki. Hasa fursa za kifedha. Pia zungumza jinsi inavyoweza kukufaidisha baadaye kimaisha.

Huenda hauna haja ya kujifunza kucheza chombo, lakini vidokezo hivi vinaweza kutumika katika mradi wowote unaotamani kuufanya.

Share your feedback