Je unajisikia hauna furaha?

Usijali ni jambo la kawaida.

Je umewahi kujikuta ukilia bila kuwa na sababu? Au kujisikia kama kifua kimekubana hivi na unajisikia kama kuna kitu kizito kimekukalia kifuani?

Unaweza kujisikia kutaka kukaa peke yako wakati mwingine na kujifikiria vibaya kuhusu wewe mwenyewe. Usijali. Ni jambo la kawaida kujisikia hivyo wakati mwingine. Haupo pekee yako na wewe bado ni wa muhimu sana.

Tunapokua tunakumbana na hisia za kila aina. Wakati mwingine unakuwa sawa, mara baadae unabadilika, halafu baadae tunarudi tena kuwa sawa. Rafiki yangu Jeni alikuja kwangu wiki iliyopita akiwa hana raha. Niliweza kumsaidia kwa sababu nilikuwa najiskia vivyo hivyo mwezi uliopita. Uzuri ni kwamba huwa baadae hii hali inapotea tu. Mwezi uliopita nilikuwa najisikia sina raha kabisa ,kwa hiyo sasa hiv nimeweza kutumia kile nilichojifunza kwa kumsaidia rafiki yangu.

Huu ndio ushauri niliompa ambao unaweza kukusaidia pia.

1. Kumbuka Mara zote kuwa kamwe haupo pekee yako

Sote tuna uzoefu wa kuwa na furaha na hata huzuni. Ni sehemu ya kawaida ya maisha. Hatuwezi kuwa wenye furaha muda wote lakini pia huzuni haiwezi kudumu milele. Unapokuwa unajisikia vibaya kumbuka unao marafiki na dada zako ambao unaweza kwenda katika ukarasa wetu na kuzungumza nae. Unapaswa pia kuwaeleza wenzako vile unavyojisikia, huwezi Jua nani naweza kukusaidia.

2. Tengeneza mpango wa kuwa na furaha. Tunapokuwa katika kubalehe hisia zetu huwa zipo juu kwa kila kitu. Hivyo ukiwa unajiandaa kukabiliana na siku ambazo zitakuwa mbaya unapaswa kuandaa mpango madhubuti wa vitu vyote unavyoweza kuvifanya kujipa rahakujisikia vizuri.Vitu hivyo ni kama kwenda kukutana na marafiki. Kwenda kuogelea, Kuangalia muvi,na Amina au kupika maandazi na akina Cesilia. Kufanya vitu ambavyo unavipenda ukiwa na watu unao wapenda kutakufanya kujisikia vizuri haraka.

3. Jifunze kuwa na moyo wa Shukrani Kuwa na siku moja mbaya haimaanishi itabaki kuwa hivyo katika maisha yako yote jaribu kutazama kwa mapana. Andika mambo matano kila siku ambayo yanakufanya kushukuru kwa kufanya hivi kunaweza kukuweka katika hali nzuri mno.

Kwa ujumla kuongea na marafiki kunasaidia sana kwa sababu hukufanya kutambua haraka kwamba haupo pekeako katika yale unayoyapitia, na kama wasichana wengine wanaweza kuyashinda wewe pia unaweza.

Share your feedback