Weka chini WhatsApp na uwaulize marafiki zako “Kuna nini?”
Intaneti ni nzuri sana! Unaweza kukutana na watu wapya, kujifunza mambo mapya, na kushiriki mawazo na marafiki kutoka kote duniani. ...Lakini itakuwaje kuhusu marafiki zako wanaoish mtaa wa hapa karibu? Tunapenda wavuti sana kama wewe, lakini ikiwa wakati wako wa kuwa mtandaoni umeanza kuweka vikwazo visivyoonekana kati yako na marafiki zako, huenda wakati umefika wa kuweka simu chini na ushuhudie dunia kwa #nofilter!
Mazungumzo Halisi
Mei, mwanafunzi wa shule ya sekondari wa miaka 16, alituambia kuwa wakati fulani alienda kwa rafiki yake wa dhati Superette Jumamosi usiku. Marafiki zake wote walikuwepo, lakini kilikuwepo kimya cha kusikitisha — isipokuwa milio ya kila mara kutoka kwenye simu ya kila mmoja! Alifahamu kuwa mambo yalikuwa ya ajabu wakati mmoja wa marafiki zake wa dhati ambaye alikuwa amekaa upande mmoja na yeye, alipomtumia SMS!
Huenda hilo likaonekana kuwa jambo la kipuuzi, lakini ni kitu ambacho wengi wetu wameshuhudia. Ikiwa umechoka kuhisi kana kwamba uko peke yako hata ukiwa na marafiki zako, hili hapa ni wazo:
Waambie marafiki zako kuwa mtu wa kwanza ambaye ataangalia simu yake ya mkononi wakati wa kukutana lazima amwimbie kila mmoja wimbo wa upuuzi. Ikiwa hilo halitawahimiza marafiki zako kuacha vifaa vyao... Labda hamna litakalotendeka! ;)
Dunia Halisi
Sisi <3 Intaneti... Kuna mengi ya kujifunza na kufanya na kufikiria kuhusu wavuti. Na unapokosa vitu vya kutafuta kwenye Google, kuna picha za paka za kuchekesha wakati wote! Lakini usiwahi kusahau kile kilicho muhimu sana: mtu aliye karibu nawe. Marafiki zako. Familia yako. Watu unaowajali.
Jifunze kutoka kwa mshairi Wiji Thukul mwenye hekima: “Ni nini maana ya maarifa ikiwa unajifungia ndani?” Kuwepo katika maisha yako ili uwe na mambo ya ‘Kupenda’ na ‘Kushiriki’ IRL, pia.
Share your feedback