Mbinu 3 za Furaha zinazoweza kuleta tabasamu usoni.
Hisia zetu zinaweza kufanana kidogo na jinsi hali ya hewa ilivyo. Kuna wakati tunajisikia wanyonge kama vile ilivyo siku za mawingu na mvua . Na siku zingine tunajisikia wenye Furaha isiyo ya kawaida na wenye kujiamini kama ilivyo siku zenye Jua.
Kurejea kuwa mwenye Furaha pindi unapojisikia kukasirika au mpweke sio jambo rahisi. Lakini INAWEZEKANA KUFANYIKA.
Hizi hapo ni mbinu 3 nzuri zinazoweka kugeuza Hali hii (kuwa ya Furaha)
Kidokezo 1 - Roketi
Hesabu kutokea 5 kurudi 1 na jifanye kana kwamba wewe ni roketi inayotaka kurushwa kwenda angani. Kama hivi: 5... 4... 3... 2...1 RUKAAA!
Unaposema "ruka", unatakiwa kuruka kweli na kwenda kufanya kitu kitakachokufurahisha. Anza na uondoe mawazo yote mabaya. Kusikiliza mziki na kucheza ni mwanzo mzuri pia. Kidokezo hiki kitakusaidia kama kweli unahitaji hamasa ya kufanya jambo muhimu.
Kidokezo 2 - Andika na Kuchana
Kama wewe sio mpenzi wa kucheza mziki basi labda ujaribu mbinu hii. Inaitwa 'Andika na kuchana' chukua kipande cha karatasi halafu andika vitu vyote vibaya unavyojisikia. Labda mtu amekuudhi, na unasikia hasira, au wivu. Sio vizuri kuficha vitu moyoni. Viandike vyote kwenye kipande cha karatasi na Kisha KICHANE. Ni moja ya kitu kizuri sana kwani inakufanya ujisikie kwamba vitu hivi vibaya havina tena nguvu dhidi yako.
Kidokezo 3 - Kioo, Kioo Ukutani
Maneno yana nguvu kubwa mno. Hivi unafahamu kwamba mawazo yako hujenga hisia zako na hisia zako hujenga matendo unayoyafanya? Hii ndio sababu ni muhimu sana kuwa na mawazo chanya na kuyasema kwa sauti.
Hivyo kila utakapoamka asubuhi, jitazame katika kioo na urudie kusema maneno haya.
Mimi najipenda
Mimi ni imara
Ninajitosheleza
Ninapendwa
Mimi ni mrembo
Mimi ni wa thamani
Mimi Nina akili
Ninalo kusudi katika maisha yangu
Ninaweza kuzitimiza ndoto zangu
Kumbuka, hakuna mtu aliye na furaha muda wote. Kujisikia huzuni ni jambo la kawaida. Kama unajisikia huzuni ni vizuri ukubaliane na Hali yako na jaribu mojawapo ya dondoo hizi ili zikusaidie kuondokana nayo. Usijifanye kana kwamba kila kitu kipo sawa ama kuzama kwenye hisia zako. Wewe kubaliana nazo halafu zipotezee yaani ziambie kwa herii hamnipati ng'o!
Share your feedback