Nilihoji "Jinsi mambo yanavyo endeshwa."
Nilipokuwa mdogo, nilikuwa nikifurahia sana wakati familia nzima tulipokuwa tukikutana nyumbani kwetu. Mimi na binamu zangu tulikuwa tukicheza nje michezo mingi ya kushindana . Mimi na kaka yangu Tony tulikuwa ndio timu bora siku zote. Kadri nilivyoendelea kuwa mkubwa, nilianza kugundua kwamba natumia muda mwingi sana nikiwa jikoni na mama kuliko kucheza nje. Ila sasa kwa upande mwingine Tony yeye, bado alikuwa anaruhusiwa kwenda kucheza,Na waala hakuna aliyekuwa anamuita kuja kutusaidia jikoni,
Hilo lilinishangaza sana – hivyo nikaamua niulize. Nilimwuliza mama yangu kwanini mimi huwa siendi kucheza nje, nabaki tu naosha vyombo ndani,Akanijibu "Mwanangu hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa".
Mmmh niliwaza sana - Hivi kweli, inapaswa kuwa hivyo? Hakuna aliyekuwa anataka kujua nilivyokuwa najisikia..Nilitakiwa tu kutii sheria. Sikilizeni, Wasichana: Maamuzi yanapofanywa na huoni kama yanazingatia maslahi yako, una haki ya kuuliza maswali. (Lakini angalia tu uwe ni wakati ambao unahisi ni salama kufanya hivyo.)
Katika hali halisi sidhani kama kulikuwa na utofauti Kati yangu na Tony, kwa hiyo ilikuwa bado inanisumbua sana. na kwavile Mama yangu hakuwa namna yoyote ya kufanya kuhusu hilo, hivyo nikamfata Tony kuzungumza nae wakati wa usiku ambapo kila mtu alikuwa ameenda kulala. Nilimueleza jinsi nilivyomisi kuwa mwanatimu mwenzake na kumueleza endapo atakuwa ananisaidia shughuli mbili tatu basi kazi zitaisha haraka. Pia nilijitolea kumsaidia kwa kazi yoyote ambayo angetakiwa kuifanya.
Siku nyingine watu walipokuja kututembelea tena, wazazi wangu walishangaa walipotuona mimi na Tony tukiosha vyombo kwa pamoja. Sasa hivi imekuwa kama utaratibu mpya nyumbani kwetu. Hakuna sheria eti kazi za nyumba nini za wasichana pekee yao. Mimi na ndugu yangu tunafanya kazi pamoja na tunashikiriana bila shida. Najivunia sana kwa hatua yangu ya kupinga na kuongea kuhusu uonevu huo.
Sisi wasichana tunastahili uhuru sawa na mtu mwingine yeyote. Hivyo ikiwa yeyote atajaribu Kukuonea, Kaa chini, Tafakari,.Jiamini. Na kuwa tayari kupinga mawazo yao. Ikiwa ninaweza kufanya hivyo, basi na wewe unaweza pia. Ikiwa unampinga mtu mkubwa kuliko wewe, kumbuka kufanya yote adabu na heshima.
Share your feedback