Kumbe yawezekana!

Jinsi ya Kukabiliana na uonevu Mtandaoni.

Intaneti ni sehemu ya ukweli kinoma!! Unaweza kujiachia kwa kuposti mambo yako unayoyapenda kama stori,mawazo yako hata vile unavyojisikia na ukawasiliana na marafiki popote duniani!

Je ni Rafiki kipenzi wa Milele dunia nzima? Ndio kabisa!!

Lakini kuna mambo unayopaswa kufahamu. Kwanza kabisa, Intaneti ni sehemu ya umma. Mambo unayo posti hapo yanaweza kutazamwa na marafiki, familia na hata watu wengine usiowajua kabisa. Usipokuwa makini, huenda ukajikuta unawakaribisha watu wenye majibu machafu na wanaokera na hata wale waonevu vilevile . Kwa hiyo sasa unapaswa kufanya nini ukijikuta katika hali kama hii?

Tulia
Usikurupuke . Usijibu. Ki ukweli, mambo yatakuwa Sawa tu. Hem vuta pumzi ndani. Haya itoe nje sasa. Ukiandikiwa maoni yenye chuki au hata kuhatarisha wewe yapuuze halafu ,iripoti hiyo akaunti , kisha wazuie wasione akaunt yako(“wabloku”)

Kama tuu katika maisha halisi , watu wanaopenda kuonea wenzao kadri wanavyokuona ukikasirika ndo unavyowachochea zaidi. Na kama ilivyo kwenye maisha wewe wapotezee tu wanaokuchukia. Usiwape sababu yoyote ya kukunyima raha ya kufurahia mtandaoni. Kiukweli wa waonevu wengi mtandani hutafuta tu umaarufu (“kiki”) mtandaoni

Haa! Wakomeshwe!
Ikiwa unamjua mtu anayekuonea nana unaonana nae kila siku shuleni mwambie aache hiyo tabia. Lakini akiendelea kukuonea, wewe wasiliana na mtu mzima mara moja kwa ajili ya msaada kama vile mwalimu au mshauri. Mtu muonevu anaweza kusimamishwa masomo au kufukuzwa shule kutegemeana uzito wa kosa lake.

Hali Inazidi Kuwa Mbaya
Ikiwa unafikiri kuwa umefanya kila kitu na bado unaonewa, kwanza kabisa, unapaswa kuwaambia wazazi wako au mtu unayemwamini kuhusu kile kinachoendelea. Pili, kuwa mpelelezi mzuri hifadhi ushahidi wote uliopo mtandani endapo utahitajika kuripoti uonevu uliofanyiwa kwa mwalimu wako au hata polisi.

Uonevu mtandaoni ni hatari sana kwa wasichana na wanawake, hivyo sote tuweke juhudi ya kumlinda kila mmoja dhidi ya waonevu wa mtandaoni na tuwe wema kwa kila mmoja wetu tuwapo mtandaoni.

Kila kitu kitakuwa sawa
Kuonewa mtandaoni kunaweza kukufanya uwe na huzuni sana,lakini wala usijali.

Jisikie tu kwamba hauko peke yako katika hili. Kuna watu wengi sana wanaokujali: walimu, wazazi, na mabesti zako. Unaweza kuwafata kama unaona hali hii imekuathiri na unahitaji wakutie moyo. Na pia jisikie kwamba kuna mamilioni ya wasichana wengine ambao wamepitia hali kama yako. Na kwa sababu wenzako basi fahamu kuwa, wanakupigania ili uishinde hii hali.

Tunaamini unaweza Binti!

Share your feedback