Je Unahitaji motisha ili uweze kusimama na kuongea?

Nukuu hizi 7 zitakuwezesha kuzungumza

Ikiwa huwezi kusema dunia itajuaje kuwa wewe upo? Wasichana, ulichonacho cha kusema kina maana! Jinsi unavyojisikia kuhusu jambo fulani kuna maana kubwa. Kusimama na kuongea ni kitu muhimu. Hapa kuna baadhi ya nukuu za kukuhamasisha kuzungumza na kusimamia mambo muhimu kwako!

"Usiposema watafikiri kuwa unaona ni SAWA jinsi mambo yanavyoenda. Kimya siku zote huchukuliwa kama hali ya kukubali. "- Sanya Parker

"Watu wengi wanaogopa kusema wanachokitaka. Ndiyo maana hawapati wanachokitaka. "- Madonna

"Usiposema hakuna kitakachobadilika. Kwa hivyo fanya mabadiliko, ili mradi tu ulijaribu ... utaona ulifanya KITU badala ya kukaa tu kimya. "- Haijulikani

"Umaskini umeendelea kuwepo katika kila jamii kwa sababu kuna mtu alikataa kusimama na kusema." - Sunday Adelaja

"Kila wakati msichana anaposimama na kusimamia anachokitaka mwenyewe, anasimama kwa ajili ya wasichana wote." - Maya Angelou

"Ikiwa unahisi kwamba kuna jambo baya, usiogope kuzungumza. Hata kama unahisi hawatakusikiliza, we sema tu. "-(Imesemwa mahali)

"Dunia inakabiliwa na mengi. Si kwa sababu ya watu waovu, bali kwa sababu ya ukimya wa watu wema. "-(Imesemwa mahali)

Natumaini haya yamekuhamasisha Ni wakati wa kusimama na kuongea sasa!

Share your feedback