Huna dada mkubwa? Wala Usijali!

Acha tukusaidie kupata watu unaoweza kuwaamini!

Mawazo yako (13)

Ni vyema kuwa na mtu wa kuzungumza naye unapokuwa na maswali, wasiwasi au maisha yanapokuwa magumu.

Kuwa na dada mkubwa au mtu wa karibu anayeweza kukupa ushauri na mtazamo mpya husaidia sana. Hata kama huna dada mkubwa, mshauri anaweza pia kukupa msaada na mwongozo sahihi.

Mnasihi ni nani?

Mnasihi ni mshauri anayeaminika na mwenye kuwajibika, unayeweza kuzungumza naye kuhusu lolote. Iwe ni kuhusu shule, marafiki zako, wavulana, familia au ndoto zako. Mnasihi anaweza kukusikiliza, akuongoze kufanya uamuzi unaofaa au hata akusaidie kupata fursa!

Hauhitajiki kumwambia mnasihi wako kila kitu kama hujisikii, lakini kuwa na mfumo huo wa usaidizi inamaanisha kama utahitaji kuongea au kupata ushauri muda wowote basa utapatikana.

Kuwa na mnasihi sio tu kwa watu wadogo, hata watu wazima wana wanasihi pia! Sio lazima iwe mtaalamu au mtu aliye mbali, mtu mwenye moyo wa kukusaidia ambae unayemwamini na una uhakika anaweza kukupa ushauri mzuri anatosha kabisa.

Jaribu kuandika Jina la mtu unayedhani anaweza kuwa mnasihi mzuri na umuombe kama atakuwa tayari kuwa mnasihi wako

Umewahi kujaribu hii Shosti? Je una mtu ambae huwa anakushauri mambo yako au huwa unapambana tu na hali yako? Dada zako wangependa kusikia kutoka kwako kwa kutupia maoni yako hapoo chini.

Share your feedback

Mawazo yako

me nadhan wasichana tupambane bila kukata tamaa

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

naendapo ukikata tamaa ndio malengo yako utayapoteza nawewe mwenyewe utayumba. BY MDADA

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

naendapo ukikata tamaa ndio malengo yako utayapoteza nawewe mwenyewe utayumba. BY MDADA

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

ndio dada anaumuhimu wake lakin kama hauna utafanyate rafik yang hamna jins hatakama huna unaweza ukawa na wapemben akakuchukulia kama mdogo wake wakuzaliwa

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Mdada asante sana kwa kuandika maoni yako,Je ulifanikiwa kusoma makala yote? Enhee wana Springster wenzako wangependa kusikia kutoka kwako ikiwa una mtu ambae huwa anakushauri katika mambo yako,Je yeye huwa wa msaada kwako? Waweza kuja kutuandika tena hapa chini.Asante

mm pia sina dada ila najiamin na kujijali kama msichana

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Make tunashukuru kwa kuandika maoni yako na tunafurahi sana Kusikia kuwa unaijua thamani yako,kwamba ni muhimu kujijali na kujiamini maana hivyo vinasaidia kukufanya kuwa Binti thabiti.Je una mtu yeyote ambae huwa anakushauri katika mambo yako? waweza kuja kutueleza tena,tungependa kusikia kutoka kwako.

Babra Nikweli kabxa make mwanamke nikujiamini ,kujijali na kujipenda

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Faraja tunafurahi kuwa umeipenda makala yetu na kuwa unatambua thamani yako kama Binti,je wewe unaye mtu ambae huwa anakushauri katika mambo yako? Unaonaje je inasaidia?Wana Springsters wangependa kusikia tena kutoka kwako.

Mimi pia nimeipenda kkweli hii stori.

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Ni kweli ni vizuri kuwa na dada mkubwaau mtu wa kuongea nae. Mimi huwa natamani kweli kuongea na mtu naomba mnitafute jamani naishi Dar es salaam mtaa wa boko .Asante

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Ndio nshakuwa na mshaur, nmejifunza mengi kutoka kwake hakika naringa na ushaur wake. Naweza pia kutoa semina kwa wenzangu. Najivunia kwa ilo

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Huncho, Asante sana kwa kutuandikia maoni yako,na tunafurahi sana kwamba mshauri uliye nae ameweza kuongeza thamani katika maisha yako.usiache kushea na wenzako unayojifunza kwani kwa hakika watanufaika pia.Kila la heri Binti