Ishinde aibu kwa sekunde 60 tuu!

Fuata njia hizi tatu.

Wote tumepitia uko –Hebu fikiria upo darasani na huelewi kinachofundishwa lakini unaona aibu kuongea.Mtu mwingine ananyoosha mkono na kuuliza swali hilohilo rahisi ambalo uliona aibu kuuliza na ghafla kila mtu anakiri kua anahitaji msaada maana somo halikueleweka kwa wote. Au ulikua umetoka na marafiki zako na ukaona mtu ambae huwa unampenda. Unataka kweli kwenda kuongea nae lakini ndio hujiamini hata kidogo!. Wasichana wengine wakianza kuongea nae ndipo unapogundua kumbe mkaka mwenyewe yuko poa ,tena rahisi kuongea nae,moyoni unajutia unasema Dah! Bora hata ningemsemesha kumbe.

Hizi hapa njia rahisi za kuweza kuishinda aibu ili uweze kuongea na kua mtu jasiri kama unavyotamani kuwa.

  1. Jiamini. Unajua muonekano unaweza kumdanganya mtu eh! kwahiyo hata kama unajisikia hauna ujasiri ndani yako kama ukiwa unamuangalia mtu kwa kujiamini,utashangazwa ni jinsi gani inaweza kukusaidia na kubadili mtizamo wako.

  2. Usifikirie sanaa! Kukataliwa kwenye maisha kupo sana. Mfano ikitokea umeuliza swali la kipuuzi mbele za watu au ukajikuta unavunja urafiki kwa sababu ya vitu ambavyo mmeshindwa kukubaliana,au hata ukajikuta umefanya kitu cha aibu mbele ya mkaka unaempenda, wala usiwaze unatakiwa usonge mbele itakufanya uwe mtu imara.

  3. Jiamini unaweza. Hata kama wewe unaepaswa kuongea unaona aibu tambua unajua unachokifanya, kwa hiyo anza kuamini uwezo wako na akili uiyonayo.Unapozidi kujiamini ndipo unapopata ujasiri zaidi.

Haya sasa nenda kajaribu kufanyia kazi hizi dondoo ,muda si mrefu utaanza kuona matokeo ya kujiamini ndani yako hadi nje.

Share your feedback