#Vibekamalote
Utani na mizaha ni jambo la kawaida kati ya marafiki. Na kwenye mitandao ya kijamii huwa tuko wabunifu sana ,–kwa picha na video za kuchekesha tunazotumiana. Lakini tusipokuwa makini, tunaweza kuwakwaza wengine bila kukusudia kwa posti zetu. Jiulize na ujibu maswali haya ili yakusaidie kuamua kama inafaa kuposti kitu fulani au la!
Je, unataka kuposti kitu cha kumtania rafiki yako?
1. Je Posti yako inagusa udhaifu wowote alionao rafiki yako?
A. Hapana (Endelea kwenye swali la 2)
B. Ndiyo (Acha kuposti)
Shogaangu ishia hapohapo. Kumtania mtu kuhusu udhaifu wake ni moja ya njia rahisi za kumuumiza mtu. Inaweza kuchukuliwa kama namna ya kumuonea au kumdhalilisha. Tujiepushe na mambo nyeti kama hayo, sawa?
2. Je Post yako ina mambo ya siri kuhusu rafiki yako ?
A. Hapana (Endelea kwenye swali la 3)
B. Ndiyo (Acha kuposti)
Uwiiii! Hii Hapana kabisa maana inaweza kumuweka rafiki yako hatarini. Wengine wanaweza kuanza kumkejeli,au kumdhalilisha kwenye mtandao. Pia, sio poa kushea mambo ya siri ya watu wengine.
3. Je Hii posti ina matusi au lugha chafu?
A. Hapana (Endelea kwenye swali la 4)
B. Ndiyo (Acha kuposti)
Kamwe Hupaswi kutumia lugha chafu za aina hiyo kwenye wall yako.Tujitahidi kutumia maneno mazuri na ya kiistaarabu tunapokuwa mitandaoni.
4. Je Una uhakika rafiki yako hatakwazika?
A. Ndio (Nenda kwenye Jibu A)
B. Sijui (Nenda kwenye Jibu B)
Jibu A: POSTI!
Inaonekana hii posti haina madhara yoyote. Endelea na bonyeza tuma!
Jibu B: Subiri Kwanza KIDOGO
Ikiwa bado huna uhakika, hebu vaa viatu vya mwenzio, ingekuwa ni wewe mtu mwingine amekufanyia hili, ungejisikia kuwa umetukanwa? Hii itakusaidia kufanya maamuzi ya busara siku zote.
Natumaini mwongozo huu umekusaidia kuhakiki posti zako. Hata kama tunataniana basi tutumie mitandao ya kijamii kwa uangalifu.
Share your feedback