Kusema HAPANA kuliokoa maisha yangu

Usiogope kusema hivyo!

Maria kutoka darasa la juu alitualika mimi na rafiki yangu Carolina kwenye sherehe na wanafunzi wengine wakubwa. Tulikuwa na raha tele huku tukicheza, tukipiga stori na kutulia. Tulijisahau na tulipokugundua na kuangalia ilikuwa karibu saa sita usiku. Tungepaswa kuondoka wakati huo ikiwa tungetaka kupata basi la mwisho kurudi nyumbani.

Maria na marafiki zake wakubwa walinisikia nikimwambia Carolina kwamba ilitubidi tuondoke ili tupate basi. Walituambia kwamba hatungeweza kuondoka, kwamba sherehe ilikuwa ndio kwanza inaanza kuchangamka. Nilimwambia hatupaswi kulikosa basi la mwisho, ama sivyo tusingekuwa na njia yoyote ya kurudi nyumbani. Walianza kutushawishi kwa kusema kuwa sisi tulikuwa tunaboa.

Carolina alinitetea na kusema kuwa kuchelewa kurudi nyumbani ndo ingeboa zaidi.

Ilikuwa wazi Maria alikuwa amelewa kiasi na hakukata tamaa. Mimi na Carolina tulikuwa tumelemewa. Tulikuwa na wakati mzuri, na hatukutaka kuonekana kama watoto na wenyekuboa mbele za wakubwa. Lakini tulijuwa kwamba kurudi nyumbanikwa miguu usiku ilikuwa hatari sana na basi ndio njia pekee iliyokuwa salama kwenda nyumbani.

Ingawaje tulikuwa na wasiwasi, mimi na Carolina tulikuwa na msimamo. Tulisema tusingeweza kuendelea kukaa tena na tukamwambia Maria na marafiki zake kwamba sisi tunaondoka. Tulikuwa na wasiwasi jinsi ambavyo Maria angeweza kufika nyumbani – hivyo tulianza kumwambia kwamba anapaswa kuondoka pamoja na sisi. Wavulana wote wakubwa walianza kucheka. Mimi na Carolina tulijua kwamba tulihitaji kumchunga Maria na hatukujali tulivyoonekana kwa wale wavulana wakubwa. Kufika nyumbani salama na kumchunga rafiki yetu ilikuwa muhumu zaidi kuliko kuendelea kukaa kwa masaa machache zaidi kweye sherehe!

Baada ya mvutano, Maria alikubali kwamba angeungana nasi na kuondoka kwenda nyumbani kwa basi.

Ingawa nilikuwa na wasiwasi kuwabishana na vijana wale wakubwa na kumwambia Maria cha kufanya, nilijua sikuwa na jinsi. . Ilibaki kidogo mno tungelikosa basi. Siku iliyofuata tulisikia habari kwamba kulikuwa na wizi kwenye barabara ambayo tungepita kwa miguu usiku huo. Kusema hapana kuliokoa maisha yetu na Maria pia alishukuru tulimpeleka nyumbani.

Share your feedback