Yeye ni kama mimi tu

Kutoka kuwa adui hadi rafiki

Nilipoanza shule ya sekondari mara ya kwanza, sikuwa nikifikiri nilikuwa mzuri sana. Nilifikiria kwamba nilikuwa mwembamba sana, na mrefu sana. Nilipenda kucheza michezo wakati wasichana wengine walipenda kununua vitu. Alama zangu zilikuwa sawa lakini sikuwa mtoto mwerevu sana.

Msichana mwingine shuleni, Beth, alikuwa kinyume nami. Hakuonekana kuwa kamili, bali alikuwa na alama nzuri sana. Walimu walimpenda na kila mtu alitaka kuwa rafiki yake. Alikuwa mkarimu kwa kila mtu, kitu ambacho kilimfanya asiwe na dosari yoyote.

Lakini sikuwa mzuri kama Beth. Wivu ulinifanya niwe mbaya. Sikutabasamu au kufanya juhudi zozote za kuwa na marafiki tulipokuwa katika darasa moja. Kwa siri nilitaka kuwa rafiki yake, hata kama matendo yangu yalionyesha sivyo.

Kisha siku moja, nilipokuwa natembea kuelekea nyumbani kutoka shuleni, nilimwona Beth mbele yangu. Alikuwa anaongea kwenye simu, na ningeweza kusikia akilia polepole.

Alipokata simu, nilijua ninapaswa kufanya kitu. Nilikuwa na wasiwasi, lakini kwa upole nikamgusa begani na nikamuuliza kama yuko sawa. Akiwa bado analia, alitabasabu na akasema, 'ndiyo niko sawa, asante'.

Ingekuwa rahisi kwangu kusema ni sawa na niendelee kutembea, lakini badala yake, nikaamua kuwa rafiki na kutembea naye

Beth akakubali. Kwa muda tulinyamaza, lakini baadaye tukaanza kuongea. Tuliongea kuhusu mambo ya kawaida, kama vile jinsi mtihani wetu wa sayansi ulivyokuwa na jinsi Bw. Turnbell asivyo mtu mzuri. Tulizungumza kuhusu mambo mazito pia. Beth alikuwa amekasirika kwa sababu rafiki yake wa kiume alikuwa amemwacha. Alimwambia kwamba alikuwa 'mnene sana'. Nikafikiria kuwa huo ni wazimu, lakini Beth akaniambia kwamba hajihisi vizuri kuhusu mwili wake.

Jioni hiyo, tulinunua aisikirimu na tukaweza kufahamiana vyema. Akaniambia kwamba wakati hajihisi ana ujasiri yeye hujitamkia maneno mazuri. Kwa sasa pale mmoja wetu anapokuwa na huzuni, sisi husaidiana kujengana kwa kusema mambo matatu mazuri.

Kwa mfano, nilimkumusha Beth kwamba alikuwa mkarimu sana, huwa anatabasamu kila wakati na ni mzuri sana katika hesabu kuliko mtu yeyote. Yeye akaniambia kwamba anapenda nywele zangu, uwezo wangu wa kucheza voliboli na yeye hufurahia wakati ninaposoma hadithi zangu kwa sauti darasani.

Ni vizuri kujiona kupitia macho ya wengine ili kujikumbusha mambo mazuri uliyonayo.

Sasa, badala ya kumwona Beth kama mtu mzuri kuliko mimi, ninaona jinsi sisi sote tulivyo wazuri kwa njia tofauti. Yeye ni mzuri katika hesabu na sayansi, mimi ni mzuri katika kuandika na historia. Hakuna yoyote aliye mzuri au mbaya - ni tofauti tu. Na sisi sote tunapenda voliboli!

Share your feedback