Unastahili mambo mazuri!
Hivi unajua kwamba akili yako ni kama ulingo wa kivita. Ni kawaida kuwa na mawazo mazuri na mabaya yanayopingana. Yote yanapigania kupata kusikilizwa. Wakati mwingine unaweza kuhisi ni kama mawazo mabaya yanashinda, lakini haipaswi kuwa hivyo wakati wote. Katika kila vita kuna mikakati ya namna ya kushinda vita hivyo ndivyo ulivyo hata wewe pia - wewe ni MSHINDI.
Hebu ngoja tujadili kidogo kuhusu hili, ili uweze kuyaepuka mawazo mabaya unapaswa kuacha tabia ya kujiona haustahili. Je wewe kama msichana upo tayari? Vizuri, sasa shika kalamu na daftari.
Hatua ya 1 - Weka mambo katika mtazamo sahihi
Tunaporuhusu mawazo mabaya kutawala akili zetu, tunaishia kusahau mambo mengine yote mazuri kuhusu sisi. Hivyo kila wakati wazo baya linapokuja kichwani tunahitaji kuuzoesha ubongo wetu kufikiria jambo moja zuri fastaa. Andika katika kitabu chako jinsi ulivyogeuza wazo baya kwa mfano hakuna mtu anayenipenda na badala yake kuwa na wazo zuri kwamfano Mimi ni mtu mwenye upendo na mwenye kujali, na watu wananipenda hivi hivi nilivyo.
Hatua ya 2 –Wewe mwenyewe Unajionaje?
Vile unavyoamini ndivyo unavyokuwa. Hivyo ikiwa unaamini huwezi kufikia malengo yako, kuna uwezekano mkubwa hutaweza kuyafikia. Badala yake, amini mambo mazuri kuhusu wewe. Kuwa na maneno ya kusema ambayo unaweza kurudia kila asubuhi. Kwa mfano unaweza kusema:
MIMI NI WA THAMANI
NINA NGUVU
NINALO KUSUDI LA MAISHA
Na hata ikibidi andika chini hata mara 100 na yaseme kwasauti ili ulimwengu usikie!
Hatua ya 3 – Sahau yaliyopita
Ni jambo la ajabu jinsi ambavyo akili zetu hujikita zaidi kuwaza makosa tunayafanya kuliko hata kumbukumbu za mambo mazuri. Kama utatumia muda wako mwingi kuwaza juu ya makosa yako itakufanya kuwa mtu usiyejiamini. Hivyo kwenye hilo daftari lako andika mambo uliyowahi kuyakosea ama makosa uliyowahi kuyafanya na kwa chini andika kile ulichojifunza kupitia hayo makosa.
ukizingatia zaidi kile ulichojifunza badala ya kosa ulilofanya kutakuongezea umakini na furaha maishani!
Kuwa na mtazamo sahihi sio jambo linaloweza kutokea ndani ya siku moja lakini chagua kujipenda wewe mwenyewe kila sikuna kukumbuka mambo mazuri kuhusu wewe mwenyewe.
Share your feedback