Ni kweli tunaweza tukawa tofauti ila wote tunapenda kuwa na marafiki.
Hivi umewahi kugundua tofauti ulizonazo na marafiki zako? Kuna wakati watafanya kichwa chako kuuma, mambo ya hapa na pale, na jinsi mnavyogombana.Lakini unapofikiria vizuri kuhusu tofauti hizi utagundua ndizo hasa zinazofanya urafiki wenu kuwa wa tofauti, unaleta furaha na mnafurahia maisha.
Pale nampokuwa mnataniana na kufanyiana maigizo tabia gani hasa huibuka kati yenu? Tumejaribu kuziorodhesha chache hapa chini. Hebu tuambie wewe unatabia gani kati ya hizi.
Dada Mkubwa
Huyu hujifanya ndo kama mama yenu. Atawatunza, mara zote atawafikiria nyInyi kwanza, yupo kwa ajili ya wanaolia na kukata tamaa. Huyagusa maisha ya wote wenye kuhitaji msaada
Kiongozi
Huyu yeye anafahamiana na kuongea na kila mtu. Huwa ni mtu rahisi kumfuata pale mwingine anapomuhitaji amsaidie ama amshauri. Atakuongoza namna unavyoweza kutengeneza urafiki kwa haraka na watu wapya.
Mtata
Huyu ndo mtetezi wa kundi. Huwa hana uoga na yupo tayari kupambana kumlinda yoyote kati ya marafiki zake. Huwa anakufanya kuona jinsi alivyo na moyo uliojaa upendo na wenye shauku ya kumlinda kila anayempenda.
Mchakarikaji
Huyu ni yule ambaye anaijua hela na kuhusu mambo ya biashara. Anajua namna ya kusaka pesa wakati mliobaki hamjui kitu. Atawafundisha namna ya kutunza pesa na namna ya kuzizungusha ili kukuza mtaji.
Mwana Urembo
Huyu huwa ni mrembo wa nje na ndani. Ni mtu unayeweza kumtegemea kwa ushauri kuhusu mitindo mbali mbali na urembo. Atakusaidia kutambua urembo wako halisi na namna ya kujipenda.
Malkia
Anapenda sherehe na huwa amejawa na stori ambazo kila mmoja hupenda kumsikiliza. Huwa anamchangamsha kila mtu hasa wale wenye huzuni. Huwa anakuonyesha kwamba nyakati mbaya huwa sio mbaya sana kama zinavyofikiriwa hasa kama umezungukwa na watu sahihi
Kila mmoja kwenye kikundi chenu ana sifa na ujuzi wa aina yake. Hivyo furahieni tofauti mlizonazo. Kuna thamani kubwa sana hata katika muda mnaoutumia kila siku kama marafiki. Utajifunza jinsi ya kuishi na watu tofauti, utakuza upendo, na utajenga fikra pana zaidi.
Share your feedback