Changamoto ya Furaha

Kupata furaha kulinifanya niache kuwa na wasiwasi

Iwapo kungekuwa na tuzo la mtu aliye na wasiwasi zaidi duniani, pengine ningeshinda! Wana Springter, mimi huwa na wasiwasi sana... Kuanzia mimi hadi ndugu zangu na mitihani, kuanzia marafiki, hadi mwili wangu, hadi mustakabali wangu, orodha ni ndefu. Daima mimi huwa natarajia mambo kwenda vibaya, na kwa sababu hiyo, mambo huwa yanaenda vibaya!

Wiki iliyopita rafiki yangu Selima alichokeshwa na jinsi nilivyokuwa na wasiwasi. Wasiwasi haukuwa unanipeleka mahali popote na alikuwa sahihi. Kila wakati nilikuwa na wasiwasi, dhiki na singeweza kuzingatia. Si vizuri!

Selima alipendekeza nijaribu kitu kinachoitwa Changamoto ya Furaha. Alinieleza furaha si kitu kinachoanguka kutoka mawinguni. Lazima uitafute sana na ufanye uamuzi wa kuwa na furaha. Pia Selima alisema kuna hatua 3 kwenye safari hii ya furaha. Hizi ndizo hatua alizonifunza kuhusu furaha:

HATUA YA 1

Ili kuanza Selima aliniuliza baadhi ya maswali ili kunisaidia kutambua ni nini ninachokipenda maishani. Aliniuliza:

  • **Wewe huota kuhusu nini?**
  • **Ni nini hukusisimua na kukupa nguvu?**
  • **Ni nini unachopenda?**

Maswali haya yalifanya niweze kufikiria na yalinisaidia kujijua zaidi. Niliweza kuandika orodha ndefu ya vitu ninavyopenda maishani.

HATUA YA 2

Baada ya kuwa na orodha yako ya furaha, andika muda ambao unachukua kufanya vitu hivyo.

Yangu ilikuwa hivi:

Kuchukua muda na marafiki – Mara 2 tu kwa mwezi kwa sababu hakuna yeyote alitaka kuwa na mimi kwa sababu nilikuwa na wasiwasi sana.

Kupiga picha maridadi – Sijawahi, kwa sababu nilifikiria kuwa sifai kuwa mpiga picha.

Kujifunza kuoka keki tamu – Mara moja baada ya muda, kwa sababu nilikuwa mvivu na kuahirisha.

WOW! Nikaanza kugundua kwamba nilichukua muda mchache sana kufanya ninachopenda na muda mwingi nikiwa na wasiwasi! Ndio maana nilihisi wasiwasi wakati mwingi.

HATUA YA 3

Selima aliniambia siri ya furaha ni kujua unachokipenda na kukifanya!! Baadaye, tulichukua miezi 12 ya mwaka na tukatengeneza mpango wa kila mwezi. Kila mwezi ningezingatia kufanya kitu kwenye orodha yangu ambacho kilinifurahisha.

Kwa hivyo mnamo Januari nilipata chupa na nikaanza kuweka akiba ya kamera. Mnamo Februari nilichukua muda zaidi jikoni na wazazi wangu nikijifunza mapishi ya ajabu. Na kila wikendi niliweka juhudi za kujiunga kwa muda ufaao na marafiki wangu na kuwa na fikra nzuri.

Ninamshukuru sana rafiki yangu Selima kwa kunifunza jinsi ya kuwa na furaha ili niweze kusema KWAHERI KWA WASIWASI.

Share your feedback