Siri ya kuwa na ari kuu

Jiamini wewe mwenyewe

Je, maisha yangekuwa yanastajaabisha kiasi gani endapo watu wote wangefafana kitabia?

Hakuna mwingine kama wewe mrembo - na hiyo ndiyo nguvu yako kuu. Upekee wako ni kitu cha kujivunia kwa hiyo usifiche asili yako ndipo uweze kuingiliana na jamii. Wakati wote watu watakuwa na maoni fulani juu yako lakini kuwa mkweli wa jinsi ulivyo kwani ndiyo siri ya kuwa na ari kuu.

Kutokana na mashinikizo mengi ambayo sisi wasichana hukumbana nayo siku hizi, ni rahisi kupotea katika hali yetu ya kutokuwa salama na kuishia kutenda yale watu wanayotaka tutende. Ili uweze kuishi kwa kujiamini lazima uwe na ufahamu mzuri wa wewe ni nani na kile unachopenda kufanya..

Hatua 1- Jitambue wewe u nani

Haya yanahusu uwezo wako na udhaifu wako Je, kiasilia wewe una uwezo wa kufanya mambo gani? Je, unafana katika mambo gani? Pengine wewe ni mtalaam wa hesabu au mchoraji mzuri au unaweza vyote viwili! Ni muhimu kujua kile unachoweza kukifanya vizuri na ukifanye kitu hicho kwa sababu kinajenga kujiamini kwako. Pia, unapojua udhaifu wako unaweza kuudhibiti vizuri zaidi na kujifunza kufanya maamuzi mazuri ambayo yanakufanya uhisi ndani yako uko salama.

Swali lingine la kujiuliza mwenyewe ni - nini hukupa nguvu? Mambo mengine yanaweza kukufanya uhisi umechoka sana ilhali mengine yanakupa nguvu na kukufanya uhisi uchangamfu. Je, unajua mambo haya ni yapi? Ikiwa huyajui, anza kufikiria na utafute mambo ambayo hukusisimua.

Hatua ya 2 - Tambua kile unachopenda na ukifanye

Kufanya kile kinachokupa furaha ni njia nyingine ya kudumu ukiwa mhalisia na mwenyewe. Ikiwa kucheza dansi kunakufurahisha basi cheza dansi utakavyo dada! kiwa marafiki wanakufanya ujihisi vibaya, basi jitenge nao na utafute wengine wanaokupa fursa ya kuwa mwenyewe. Kufanya kitu unachopenda hukufanya uhisi kujiamini na unapokuwa unajiamini uwezo wako hautakuwa na mipaka.

Kufuata ndoto zako kunaweza kukufungua macho ujione ukiwa mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu ndoto zetu msingi wake ni yale mambo tunayoyapenda sana mioyoni mwetu. Kila mtu ana ndoto tofauti kwa maisha yake kwa hiyo hakikisha unachukua hatua ili utimize ndoto zako. Ikiwa ndoto yako ni kuanzisha biashara yako basi anza kutenga pesa ili uianzishe; kwa sababu ukifanya hivyo hutaweza kuzuiliwa na chochote.

Share your feedback