Unapaswa kuamini hivyo
Kuwa jasiri haimaanishi kuwa hauna udhaifu ama wasiwasi wowote. Unapaswa kuyakubali mapungifu yako na kutokuyaruhusu yakuzuie kuyafikia malengo yako ama kuishi maisha unayoyatamani.
Watu wengi wakariri na kusema vitu kwa ujumla kama vile "kuwa na hasia kali ni udhaifu" au watu dhaifu hawawezi kuwa na mafanikio "lakini hii haina ukweli wowote.
hizi ni njia zitakazokusaidia kupambana na udhaifu ulionao na kuwa jasiri zaidi:
kubali udhaifu ulionao
Wengi wetu huwa tunajihami sana pale madhaifu yetu yanapoguswa. Huwa tunafikiri watu hawatotuheshimu kama tutaonyesha dalili za udhaifu. Lakini tunakosea sana.
Ukweli ni kwamba, tunapokubali udhaifu hutujengea nguvu ya kukabiliana nao. Na hakuna anayeweza kuitumia kutuumiza mpaka tuwaruhusu wenyewe. Kukubali udhaifu wako kutakufanya uwe tayari kukabiliana na matokeo, na hii itakufanya kuwa jasiri na mwenye amani na maisha yako.
zungumza kuhusu madhaifu yako
Watu wengi huhamasishwa na matendo yako, lakini hujisikia karibu yako zaidi kama wataona udhaifu wako. Kujieleza jinsi unavyojisikia hukufanya watu kutambua madhaifu yako, hii huwafanya wawe karibu yako kwani historia za maisha yenu zinafanana. Hauko pekeako. Kila mtu hupitia unachokipitia. Hauko mwenyewe.
Watu wanapolinganisha historia ya maisha yao na yako huwafanya muwe na ukaribu zaidi. Hukufanya kuonekana mkweli na halisi. Mahusiano mazuri na watu wengine yatakufanya kuwa na furaha na jasiri, hivyo usiogope kusema jinsi unavyo jisikia hasa.
piga kazi hata kama unajiona dhaifu
Ujasiri maana yake hasa ni sikia uoga ila usiache kutenda. Kuonyesha madhaifu yetu kutaonekana kama udhaifu pale tutakapo yaruhusu yatuzuie kufanya kazi. Kama utaendelea kupiga hatua, utaendelea kujenga ujasiri zaidi. Kwa mfano, yawezekana ni muoga wa kuongea mbele za watu lakini bado unanyoosha mkono darasani bila kujali, au yawezekana hujui namna ya kufanya kitu kwa asilimia 100% lakini bado unajairibu fursa bila kujali.
Ukiwa tayari kuyakubali madhaifu yako na kuyafanyia. Kazi unaweza kuyageuza yakawa vitu vinayokupa nguvu. Hivyo usiwe mwepesi kufikiri kuwa na hisia za haraka au kuwa dhaifu ni kikwazo. Unapokubali na kuuzungumza, na kuyafanyia kazi itakusadia kuwa na nguvu na utajenga ujasiri.
Share your feedback