Mawasiliano sahihi mtandaoni ni yapi?

Unaweza kujificha kwa Kutumia jina "feki", lakini Ustaarabu ni kitu muhimu sana.

Intaneti ni sehemu nzuri sana ya kuwasiliana na kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali, lakini kumbuka: Bado kuna mtu kama wewe tu ambae huwa upande mwingine wa kompyuta.

Ustaarabu unahitajika kila mahali, ikiwemo kwenye Intaneti.Timiza jukumu lako katika kuhakikisha unaweka mazingira ya mtandaoni kuwa salama na kila mtu kufurahia ,kwa kuwa raia mzuri yaani (Intaneti + raia), Haya basi! Tuanze na vidokezo hivi vya Mawasiliano sahihi mtandaoni (Intaneti + tabia ya kistaarabu).

“Jina Lako ni Nani?”
Kwenye mitandao ya jamii, huenda rafiki kipenzi akawa anajulikana kama ‘KewlGirl2002’, lakini kumbe ki uhalisia yeye ni Ana, Lisa au Miriam. Wasichana wengine hugundua namna walivyo wabunifu wanapoingia mtandaoni, na yule ambae huwa na aibu,utashangaa anabadilika ghafla anakuwa mtu wa kuchat hujawahi ona.

Kumbuka: Kuwa mwangalifu hasa kwa taarifa zinakuhusu(wasifu wako) Kamwe huwezi kumjua mtu halisi unae wasiliana nae,hivyo basi usiposti au kusambaza picha au mambo yako binafsi kwa watu usiowajua. Inasemekana kwamba hapa duniani, asilimia 99 ya watu ni wazuri na wa kawaida tu — lakini hilo halimaanishi usiache kujilinda!

Pia kuwa mwema, utu wako wa mtandaoni unaweza kuwa tofauti kabisa na jinsi ulivyo lakini kamwe usiwahi kumwambia mtu kitu ambacho huwezi kukisema kwake ana kwa ana.

“NIMEKASIRIKA SANA!"
Wakati mwingine watu watakuwa wajeuri na wenye maudhi kwenye Intaneti. Usiruhusu wakuudhi. Kutumia lugha mbaya na za matusi mtandaoni sio kwamba ndio sehemu nzuri zaidi kuliko mtaani. Posti yenye ujumbe ulio andikwa kwa herufi kubwa tu na alama ya mshangao hudhihirisha ya kuwa wewe huongea kwa makelele na Jazba wakati wote.Hata hivyo haiwezekani kuwa huwa unamuongelesha mwenzio shuleni kwa kelele,kwa hiyo usifanye hivyo mtandaoni.

Lakini utafanyaje endapo ukijikuta kwenye malumbano mtandaoni? Kwanza kabisa jipe muda wa kuvuta pumzi ndani halafu tulia.Tafakari namna ambavyo ungemjibu huyo mtu kama ungekuwa nae ana kwa ana badala ya mtandaoni.

Mwandishi wa habari Fatma Rajab ni mfano bora kuhusu jinsi ya kukabiliana na malumbano kwenye dijitali. Akiwa kama mwandishi wa habari, na mtu mashuhuri kwa umma ,kuna watu ambao hawamkubali naye na hawafurahii hata kidogo. Hata watu wanapoandika maoni ya kuleta karaha au kumkerera kwenye Twitter, Kamwe huwa haanzi kuwatusi na kuwashambulia. Ana ujasiri wa kupuuza watu wengi wanaomshambulia mtandaoni. Ni mfano bora kwa wasichana kila mahali kuhusu wakati gani na namna unavyopaswa kuandika maoni yako na wakati gani uwapotezee tuu.kwa sababu hata ufanyeje wanaokuchukia watabaki kuwepo tu,na haina haja ya kuwachukia kwa sababu wewe uko tofauti au siyo?

Share your feedback