Ni wakati wa kuvunja ukimya
Baadhi ya mazungumzo ni magumu kujihusisha nayo, kwa mfano nini ambacho ungetaka kusomea au kufanya utapokua mkubwa, na ni wakati gani ni sahihi wa kujamiiana, ama kuwa na mpenzi. Iwe kwa marafiki,wazazi, mpenzi au mwalimu Kuwa muwazi kuhusu haya mambo ni muhimu sana katika maisha yako na ni jambo zuri sana.
Zifuatazo ni dondoo 5 zinazoweza kukusaidia kujua namna ya kuanzisha mazungumzo yanayoweza kufanya usikilizwe.
Usifikiri utaonekana mbabe
Usiogope kuonekana mbabe kwa kueleza jinsi unavyojisikia ama kile unachotaka. Mara nyingine sisi kama wasichana huwa tunachukuliwa kuwa wakimya na wapole na wa kutokufanya fujo. Usiogope-wasichana pia wanaweza kuwa wachangamfu na waongeaji kama walivyo wavulana, hivyo hutakiwi kujisikia mnyonge ili kuwafanya wengine wajisikie vizuri.
Maoni yako ni muhimu
Hakuna mtu mwingine duniani ambaye anaweza kuwa ulivyo zaidi kuliko wewe mwenyewe! Na hilo ndio jambo la muhimu. Jiamini kwamba sauti yako na maoni yako katika kila kitu ni muhimu. Kama utaamua kujikita na kupiga kitabu badala ya kujiingiza katika mahusiano kama wafanyavyo marafiki zako fanya hivyo. Kama unapenda mziki wa taratibu kuliko ule wa ku rap usisite kuwaeleza marafiki zako.
Tuliza hisia zako
Wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kujieleza hasa pale hasira zinapokuwa zimepanda. Pale unapokuwa na mzozo na mzazi au mwalimu unapaswa kukabili hali hiyo kwa utulivu hii itawafanya wakuone kuwa umekomaa kiakili.
Jifunze kusema HAPANA
Kama hujisikii kufanya kitu fulani, iwe ni kutoroka nyumbani au shuleni, ama kuingia katika kufanya kitu kipya na mpenzi wako, au labda hujisikii kwenda sehemu yoyote kwa sababu umechoka na kazi za shuleni. Kumbuka kuwa unaruhusiwa kusema hapana. Kwa kusema hapana kunaweza kuwasaidia wasichana wengine kusema hapana pia.
Saidia wasichana wengine
Unaposikia msichana akizungumza jambo ambalo ni muhimu kwake na ukaona kuna mvulana anamkataza, jitahidi kuwaambia vitu kama vile ‘’ nadhani kitu alichokiongea Sarah ni kitu kizuri sana’’ au unaweza kusema ‘’ wazo la Sarah ni zuri sana’’ ukiwasaidia wasichana wengine kupaza sauti zao itakusaidia wewe pia.
Share your feedback