Uwezo wako wa Kipekee

Hivi umewahi kujua una uwezo wote huu ndani yako?

Mambo!

Tunataka kukueleza siri kubwa. je uko tayari? Sawa, hii hapa.

Maisha sio rahisi, asikwambie mtu, tunaelewa jinsi unavyojisikia. Kila wiki huja na changamoto zake na changamoto hizi hutuacha chaguzi mbili. Kukata tamaa, au kupambana kusonga mbele.

Je, ni chaguo gani unafikiri mtu anapaswa kuchagua? CHAGUO LA 2, bila shaka! Msichana yeyote anaweza kujisikia kukata tamaa, lakini anakuja kukumbuka kuwa ana nguvu za kipekee zilizomo ndani yake.

Unaweza kuwa unawaza, "Mimi? Nguvu za kipekee? Haiwezekani, mimi ni msichana wa kawaida tu." Wewe si wa kawaida . Ikiwa unasoma makala zetu mara kwa mara , basi una uwezo fulani ambao utakupa nguvu ya kushinda changamoto nyingi.

Uwezo wa kipekee wa 1: Una UJASIRI

Kuwa hapa inakupa sababu 101 za kujiamini. Unapojiamini, inakupa ujasiri unao uhitaji kushinda vikwazo na kubadilisha jamii yako. Kamwe usisahau kuwa wewe ni wa thamani na maisha yako si ya bure tu,kuna kusudi maalum ndani yake.kwenye maisha yako. Unaweza ukaonyesha ujasiri wako zaidi kwa kwa kuamini uwezo na vipaji ulivyonavyo ndani yako ,kwa kuweka bidii katika kuvifanyia kazi ili kuvikuza na kuvi imarisha zaidi, visikae tu. Na kuvitumia kuwasaidia wengine.

Uwezo wa kipekee wa 2: Una NGUVU YA KUSHINDA

Ikiwa unahisi kama jambo fulani haliwezekani, kumbuka mambo yote ya makubwa ambayo wasichana kama wewe wanafanikiwa kuyafikia kila siku, kote ulimwenguni! Ikiwa wanaweza kufanya hivyo,hata wewe unaweza pia. Hivyo unapokumbana na changamoto kubwa, usisahau kamwe uwezo ulio ndani yako ambao unatokana na kuwa msichana.

Uwezo wa kipekee wa 3: HAUKO PEKE YAKO

Wakati unapopitia nyakati ngumu, unaweza kupata msaada kutoka kwa marafiki, familia na Wasichana wenzako – hustahili kupitia changamoto hizo peke yako. Tuko hapa kwa ajili yako! Ikiwa itafika wakati unahisi kama unaelemewa na changamoto, kuomba msaada ni jambo la maana sana!

Share your feedback