Jinsi ya kuwa hodari katika jambo hilo ambalo daima umetaka kijifunza!
Je, una kitu ambacho umetaka daima kujifunza lakini hujawahi kupata nafasi? Pengine ni kupamba keki, kucheza gitaa, kucheza dansi katika maonyesho, kupaka picha rangi au kukuza mboga zako mwenyewe.
Tatizo ni, hujawahi kuwa na ujasiri wa kufanya hivyo. Sasa ni wakati mzuri wa kujiamini na kuruhusu talanta yako kung'aa. Ikiwa kwa mara ya kwanza hautafanikiwa, jaribu, jaribu, jaribu tena. Tunapenda msemo huu kwa sababu huzungumzia kutokufa moyo!
Jaribu vidokezo hivi na uanze leo:
Mtafute mtu unayemjua au kumpenda ambaye ana kipawa cha kile unachotaka kujifunza. Mwulize kama angependa kukupatia ushauri au akuruhusu umwone kwa siku chache ili upate maelezo ya thamani ya mambo anayofanya. Usiogope kuuliza maswali mengi, hata kama unafikiri ni maswali ya kipumbavu.
Tafuta mafunzo mtandaoni au tafuta kozi katika eneo lako ambalo unaweza kuhudhuria. Utashangazwa juu ya mambo mengi unayoweza kujifunza kutoka kwenye mafunzo ya mtandaoni na mara nyingi huwa ni ya bure! Ikiwa inawezekana kwako, kuhudhuria kozi kunaweza kufungua milango mingine pia, unaweza kukutana na watu wazuri sana na pengine kupata nafasi ya kuwa mkufunzi au kupata ajira.
Kumbuka kwamba mtu unayempenda hakuzaliwa akiwa mzuri katika kipawa chake, alijitahidi kwa bidii ili kujifunza ustadi wake na kufika pale alipo leo. Huenda kuna wakati katika maisha yake ambapo hakuwa na motisha au kuna wakati kila mtu alikuwa bora kumshinda, sisi wote tuna siku hizo. Jambo muhimu katika mafanikio ni kuendelea hata katika wakati ambao kuna changamoto na nyakati ngumu na usife moyo.
Ielezee familia au mhudumu wako kuhusu ujuzi unaotaka kujifunza, kwa nini unaupenda na utakachofanya ili kujifunza mengi. Njia nzuri ya kutengeneza uhusiano nao ni kuwaomba msaada wakati unapokuwa na uhitaji, au waeleze utashukuru kwa mchango wowote amba wanaweza kuutoa.
Kwa hiyo, kwa kuwa sasa umeamua utakuwa hodari katika ndoto zako, kumbuka kwamba sisi sote tuna siku nzuri na siku mbaya. Lenga uzuri, sahau ubaya na umwonyeshe kila mtu jinsi ulivyo na kipaji!
Share your feedback