Unahitaji marafiki?

Basi kama ndivyo, kuwa rafiki mwema kwa wengine.

Mawazo yako (1)

Marafiki husaidia kuyafanya maisha kuwa ya furaha na kushiriki kubeba mizigo ya matatizo yako. Haijalishi idadi ya marafiki uliyonayo. Jambo la muhimu zaidi ni wewe kuwa rafiki bora kwa watu wako unaowathamini. Zipo njia nyingi mno zinazoweza kukufanya kuwa rafiki bora. Zifuatazo ni baadhi tu ya mbinu.

  • Kanuni ya msingi ni kutambua kile unachokitamani ama ambacho ungependa kukipata kutoka kwa rafiki--na wewe uwatendee kile unachopenda kufanyiwa.
  • Kuwa msikivu na heshimu mawazo ya wengine hata kama mawazo yao yanatofautiana na yako. -wakubali kwa jinsi walivyo. Marafiki wazuri huwa hawawakosoi wenzao Mara kwa mara ama kujaribu kuwabadilisha. Wafurahie marafiki zako kwa jinsi walivyo na uwatendee vile unavyopenda kutendewa.
  • Kuwa muelewa na mwenye kusamehe. Kila Mara jaribu kuwa kwenye viatu vya marafiki zako, sote huwa tunafanya makosa.
  • Kuwa muaminifu. Hii inamaanisha kufanya kile ulichoahidi kukifanya na kamwe usifanye lolote kwa kusengenya marafiki zako. Usitangaze siri za marafiki zako, labda pale tu wanapokuwa katika hatari. Kama wapo katika hatari na wanahitaji msaada tafuta mtu mzima unayemwamini ili uongee nae.

Share your feedback

Mawazo yako

kuwasifu marafiki zako

Machi 20, 2022, 8:25 p.m