Mambo 3 muhimu kila msichana anapaswa kujua…

Hakuna hedhi ambayo ni “ya kawaida”!

Kuanzia kuchagua bidhaa sahihi kwa ajili ya hedhi mpaka namna ya kukabiliana na mabadiliko yako ya hisia – hedhi inaweza kuonekana kama kitu kinachokera Lakini haipaswi kuwa hivyo. Hapa kuna baadhi ya ukweli kuhusu hedhi yako ili kukusaidia kukabiliana nayo:

1. Pata kujua kinachoendelea katika mwili wako.

Kadri unavyoendelea kufahamu zaidi juu ya nini unachopaswa kukitarajia katika hatua tofauti za mzunguko wako, inakuwa rahisi zaidi kufuatilia. Katika hatua za mwanzo za hedhi yako, homoni zako huunda mayai kwenye ovari zako. Katika awamu inayofuata, ovari zako hutoa mayai haya. Wakati huo huo, homoni zako zinasaidia kujenga ukuta wa sehemu ya ndani ya tumbo lako la uzazi, ili kama mayai yako yatarutubishwa (na mbegu ya kiume), linakuwa tayari kujiandaa kwa ujauzito. Ikiwa mayai hayakurutubishwa, ukuta huu unaondolewa kupitia njia ya uke kama ute uliochanganyika na damu (hedhi yako). Ndivyo inavyokuwa– sio kitu cha kutisha au kigeni, mwili wako ni wa pekee na unaendelea kufanya mambo ya kushangaza!

2. Kuvuja damu – Kipi ni kawaida?

Ingawa inaweza kuonekana kama kuna Uchafu kwenye chupi yako, wala hauvuji damu nyingi kama inavyoonekana. Kiasi cha wastani cha damu ni vijiko vidogo vya chai 2-4 kwa hedhi yako yote. nyingine ni ute na tishu. Kama utashitushwa ama kudhani damu inatoka nyingi wasiliana na daktari.

Kwa miaka michache ya mwanzo ya hedhi yako, mizunguko kidogo itakuwa siyo ya kawaida. Baadhi ya miezi utaona damu nyingi na, miezi mingine utaona kuwa ni nyepesi.

3. Mabadiliko ya hisia huwa ni kweli na sio maigizo.

Je unajisikia kama una uchovu mwingi zaidi, kuvimbiwa au mwenye kukasirika haraka kabla ya hedhi yako? (dalili za awali za hedhi) ndio jina la mabadiliko ya kihisia na ya kimwili kwa mwili wako kabla ya hedhi. Homoni na mabadiliko mengine ya kikemikali katika ubongo wako husababisha haya, hivyo nenda polepole tu na mwili wako..

Zaidi ya yote – Furahia safari yako ya hedhi. Hakuna hedhi mbili zinazofanana na unapaswa kufanya ambacho kinafaa zaidi na kuimarisha mwili na akili. Jitunze wakati ambapo mwili wako unafanya unashughulika kufanya mambo mazuri!

Share your feedback