Je, mimi ni Bikira?

Nani huamua? Wewe mwenyewe!

Je, mimi ni bikira? Ikiwa umeshaanza kujaribu haya mambo au unataka tu kujua,MwanaSpringster kuna uwezekano umewahi jiuliza swali hili. Lakini usijali - tunayo majibu kwa ajili yako! Ni wasichana wachache tu ambao wanajua hili, lakini hakuna tafsiri MOJA ya neno ubikira...

Kama hakuna tafsiri sahihi, basi inaonesha kila mtu ana maana yake kuhusu.ubikiraHii inaweza kushangaza lakini ni ni habari njema kwasababu ubikira Unaweza kuwa jinsi yoyote utakavyo wewe. #MwiliWakoChaguoLako

Hakuna mtu anayeweza kujua ikiwa mwanamke ni bikira au la. Hata madaktari. Sasa inawezaje kuwepo tafsiri?Najua inashangaza si ndio?

Acha tuendelee kufuatilia. Wengi husema ubikira huondoka ikiwa uume utavunja kizinda (hymen) ndani ya uke. Hii inamaanisha kwamba msichana si bikira tena baada ya kufanya ngono na mvulana. Acha tufafanue hili zaidi:

  • Uume ni ogani ya mwanamume
  • Uke ni ogani ya mwanamke
  • Kizinda (hymen) ni ngozi nyembamba sana ndani ya uke ambayo wanawake wengi, lakini si wote, wanazaliwa nayo.
  • Ngono hufanyika pale uume unapoingizwa ndani ya uke wakati wa kufanya mapenzi.

Ni vizuri kujua kwamba kizinda (hymen) kinaweza kuchanika unapofanya shughuli za kawaida, kama vile kucheza na sio kufanya mapenzi tu. Sasa hebu fikiria wewe unacheza mchezo wa kupigana kisha unachana kizinda (hymen) chako. Kweli inamaanisha wewe si bikira tena? Inashangaza kidogo, hapana? Basi kuchanika kizinda (hymen) haiwezi kuwa njia tunayotumia kubaini ubikira.

Na je wavulana nao? Kuna njia ya kujua ikiwa wao ni bikira?

Kimya. Anafikiri, fikiri, fikiri. Anashusha mabega…

Kama ilivyo kwa wasichana, hakuna njia ya kubainiikiwa mvulana ni bikira. Hii ni sababu nyingine ya kutia shaka maana ya ubikira.

Kama ilivyo kwa vitu vingine maishani, “Ubikira” umetumiwa sana na watu ili kuwaelezea na kudhibiti wanawake na wasichana. Hata hivyo, kama kila kitu kuhusiana na ngono, wewe ndiye unayefanya uamuzi. Bikira au si bikira, nani anayejali? Kuna mambo ya muhimu zaidi ya kuwaza katika maisha yako. Kama vile kufikia malengo na ndoto zako.

Oh na USISAHAU kamwe…Haijalishi vile wengine wataongea, wewe ni wa thamani na una kusudi na hakuna yeyote anayeweza kuondoa hilo. Pia una nguvu za kufanya uamuzi wa binafsi kuhusu ni nani atakuwa mpenzi wako na mtafanya nini na lini.

Share your feedback