Kwanini kila mtu ananicheka?
Hivi karibuni nilipata changamoto kubwa sanaa shuleni kwangu. Wasichana wengine walikuwa wakinitania kila siku, sababu tu naonekana tofauti kulingana na wao. Na karibia kutimiza miaka 14 - lakini wanasema naonekana kama mtoto wa miaka kumi!
Hii ilinifanya nijiulize, “Hivi mimi ni wa kawaida? Kwanini ni mimi tu ninaye onekana tofauti? Sababu tu sina maziwa, wala chunusi basi kila mtu ananicheka! Matani yalizidi mpaka nikawa sipendi kwenda shule tena.
Siku moja nilijifanya naumwa, sikukwenda shule, na kuitumia siku nzima kusoma hadithi za Springster kwenye mtandao. Nilijifunza kuwa balehe ni kipindi cha makuzi toka utoto kwenda utu uzima. Katika kipindi hicho mwili wa wasichana unabadilika, umbo linakuwa la mviringo, mifupa ya mapaja inatanuka na wanaanza kupata hedhi kila mwezi. Kila mtu anapitia balehe katika umri tofauti. Kwa wastani wasichana wanabelehe katika umri wa miaka 10 - 14, lakini siyo wote, wengine huwahi au kuchelewa zaidi. Nilifurahi kujua kuwa mimi ni mtu wa kawaida kabisa!
Maelezo hayo kuhusu mwili wangu, yalinifundisha kuridhika na jinsi nilivyo na kuamini mchakato mzima wa kubadilika. Kukua ni safari na kila mtu ana safari yake tofauti. Kwahiyo badala ya kujilinganisha na wengine inabidi kufurahia vitu uilivyonavyo. Bila mwili usingeweza kupumua, kula au kutembea. Kwahiyo kuna haja ya kufurahia na kuthamini mwili wako bila kujali unaonekanaje. Kusoma jinsi mwili wangu unavyofanya kazi kulinisaidia kujua ukweli na kubadili mtazamo wangu.
Kwahiyo sasa naupenda mwili wangu na kuuongelea vizuri. Nilipata ujasiri wa kwenda shule siku iliyofuata. Kama kawaida walianza kunitania, nilisimama na kuwaambia kwa ujasiri, “Sababu tu sijaanza hedhi, sijaota maziwa, sijanenepa wala kurefuka haina maana kuwa mimi siyo mtu wa kawaida. Napenda mwili wangu na nina furahi kuuacha ubadilike wenyewe kwa wakati wake.”
Niligundua sihitaji kuweka akilini maneno yao ya kuvunja moyo kwanza hilo ni tatizo lao siyo langu. Baada ya kuongea nao hayo waliacha kunitania na kugundua kuwa najua vitu vingi kuhusu balehe. Walitaka kujua nimejifunza wapi vitu vyote hivyo, niliwaambia, “Nasoma hadithi za Spingsteri.”
Share your feedback