Stori za kizushi kuhusu hedhi.

Tunazianika zote hapa kwa ajili yako.

Tanzania kuna baadhi ya watu huamini Kuwa ikiwa upo kwenye siku zako basi ukichuma tu mboga lazima zikauke.Nchini India, wanawake wengi hupigwa marufuku kwenda maeneo ya ibada wakati wakiwa kwenye siku zao. Nchini Marekani, watu huwa wanasema usiende kuweka kambi porini maana utawavutia dubu wakufate. Nchini Afghanistan, baadhi huamini kuoga wakati wa hedhi kutakusababishia kuwa mgumba, na huko nchini Australia wanasema usije ukathubutu kwenda kuogelea baharini maana papa watasikia harufu ya damu yako ya hedhi na kukuua.

Haya yote sio ya kweli. Kwa karne nyingi kumekuwa na habari nyingi za uongo zilizosambaa na kuaminiwa na karibu nusu ya idadi ya watu waliopo duniani – hedhi.

Hedhi yako sio tu kwamba ni hali tu ya asili lakini pia ni kitu kizuri sana. Zifuatazo ni njia unazoweza kuzitumia kukabiliana na fikra potofu kuhusu hedhi.

UZUSHI: Kuna hedhi ‘isiyo na shida na yenye shida’

Kamwe huwezi kupata hedhi zinazofanana kila mwezi. Hedhi hutokea kila badaa ya siku 21-45, na hudumu kutoka kwa siku 2-7, damu ya hedhi inaweza kuwa nzito au nyepesi, wakati mwingine inaweza kuchukua hadi miaka 6 ili kuwa na mzunguko wa Unaoleweka.

Kuna vitu mbalimbali vya kutumia wakati wa hedhi yako. Kama vile – pedi, kanga, vikombe maalum vya hedhi au chupi za hedhi. Usisikilize stori za mtaani eti kwamba kuna bidhaa ambazo ni safi na bora zaidi au zinafaa kuliko zingine. Wewe kuwa mjanja halafu fanya kile ambacho ni sahihi na usiache kujiamini pia.

UZUSHI: Hedhi ni Kitu kibaya sana

Sio kweli. Badala yake wewe jaribu kuwa na mtazamo chanya kuhusu hedhi. Badala ya kuona hedhi yako kama kero, jaribu kubadilisha mtazamo wako na uone kuwa ni kitu cha kawaida. Hedhi yako ni ishara ya kuwa na afya njema na ya kuwa viungo vyako vya uzazi vinafanya kazi. Kwa hivyo wakati mwingine utakapoona damu ya hedhi hakikisha umejiandaa vizuri "kumpokea mgeni wako" hata kama ni mchafu!

UZUSHI: Hedhi ni kitu cha Siri

Hakuna chochote cha kuficha! Badala yake, vunja ukimya,haijalishi kama ulivunja ungo kitambo au hujavunja. Tuzungumze na ndugu au marafiki zetu kuhusu kile tunachokipitia kila wakati. Hili litawasaidia wasichana wengine wanaokuzunguka kutokuwa waoga wa kuongea kuhusu hedhi zao.

Hakuna haja kumuonea aibu mtu –usiruhusu hedhi ikakunyima raha ya maisha!

Share your feedback