Ni kile kipindi cha kila mwezi tena
Ni kweli ni kile kipindi cha kila mwezi tena lakini hedhi zote hazifanani. Na sio Mara zote utakuwa na hisia zile zile uwapo katika hedhi. Katika baadhi ya miezi hedhi inaweza kuwa bila shida yoyote Ile. Na miezi mingine unaweza kupata maumivu.
Lakini usiwe na wasiwasi hizi hapa ni dondoo 3 zitakazo kusaidia kufanya hedhi yako isiwe na shida kadri inavyowezekana pindi utakapopata.
Usifanye: usile vyakula vya mafuta, chumvi na vyakula vya sukari.
Ni vyakula vinavyojulikana kuongeza Hali ya kuchoka, tumbo kujaa gesi, hofu, na hisia kubadilikabadilika. Pia vyakula hivi vinaweza kusababisha matiti yako kuwa na maumivu makali.
Kitu kingine cha kukiepuka. Vyakula vilivyotengenezwa kwa maziwa. Maziwa yana madini ya kalsium na yanavirutubisho. Lakini sio vyakula rafiki unapokuwa katika siku zako kwani huongeza maumivu na kujaza tumbo gesi. Hivyo ni vyema kukaa mbali na unywaji wa maziwa mpaka hedhi itakapoisha. Ni kweli kwamba kuepuka ulaji wa vyakula hivi ni rahisi kwa maongezi kuliko matendo hasa kama unavipenda. Lakini unaweza.
Fanya: kula samaki, mboga mboga na matunda.
Vyakula hivi vitakusaidia kukupa hisia nzuri na kuboresha afya yako. Kunywa kikombe cha Chai ya tangawizi unaweza kuchanganya na asali. Hii husaidia kupunguza maumivu ya tumbo la hedhi. Kama unatokwa na damu nyingi, kula vyakula vyenye madini chuma kama vile maharage na mboga za majani kukusaidia kubakia mwenye nguvu. Pia, kunywa maji mengi.
Usifanye: Epuka kunawa na kujisafisha.
Katika baadhi ya maeneo wasichana huambiwa hawapaswi kunawa wawapo kwenye siku zao kwa sababu wanaweza kunajisika au kuwa wagumba lakini hili halina ukweli wowote. Hii ni moja ya mawazo potofu kuhusu hedhi.
Fanya: Nawa Mara kwa mara na kuwa msafi.
Unapokuwa katika siku zako ni muhimu mno kuwa msafi na kuosha sehemu zako za siri kwa maji. Hii itakusadia kuondoa harufu yoyote mbaya ama kuruhusu bakteria kuzaliana. Unatakiwa kubadili pedi kila baada ya masaa 2-4 na tupa pedi zilizotumika kama inawezekana. Kama umetumia kitambaa basi hakikisha umekifua na kukianika Mara kwa mara.
Usifanye: Usivae nguo nyeupe.
Kama huwa upo hatarini kujichafua unapokuwa katika siku zako, epuka nguo nyeupe au zenye rangi zinazong'aa. Hii itakuepusha kujiangalia kama umechafuka kila Mara. Unastahili kuwa na mawazo tulivu uwapo katika siku zako.
Fanya: Vaa nguo zenye rangi nyeusi.
Itakufanya kujiamini na kuwa na utulivu. Na kama ikitokea ukachafuka haitokuwa rahisi kwa mtu mwingine kugundua. Unaweza kunyata na kwenda kubadili nguo kama itahitajika.
Kumbuka: Haikuzuii kupata mimba ama magonjwa ya zinaa kama utafanya ngono uwapo kwenye siku zako.
Kuna swali lolote? Ongea na mtu mzima unayemwamini kama vile dada yako, shangazi au mhudumu wa afya mwenye uzoefu.
Share your feedback