Usiruhusu hedhi yako kuwa kizuizi

Jiamini. Usiwe na hofu.

Kwa kawaida hedhi huambatana na maumivu, chunusi, kubadilika kwa hisia na kuaibika LAKINI, niko hapa kukuambia kuwa haiwi hivyo kila wakati.

Unapokuwa katika siku zako, watu wanaweza kukuambia kila aina ya mambo kama vile "baki kitandani siku nzima", "usicheze michezo", au "usimwambie mtu yeyote kwamba upo kwenye siku zako", lakini hauhitaji kuwasikiliza. Ikiwa unajisikia vizuri kufanya kitu, kifanye. Usimruhusu mtu yeyote kuwa kizuizi, binti! Shukrani kwa Springster, sasa huu ndiyo mtazamo wangu kwa kila kitu katika maisha.

Mwezi uliopita nilikuwa na mchuano mkubwa. Kila siku mimi na timu yangu tulifanya mazoezi. Tulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda michuano ya taifa katika mbio za kupokezana. Kila kitu kilikuwa shwari tukikaribia mchuano. Lakini siku moja kabla, katikati ya mazoezi niliingia katika siku zangu bila kutarajia!

Uzuri sikupata madoadoa yoyote, lakini nilihitaji kuondoka mazoezini mapema ili kupumzika kabla ya siku iliyofuata. Ni mama yangu pekee aliyejua kuhusu siku zangu na niliona aibu kumwarifu kocha wangu wa kiume kwamba nilikuwa katika siku zangu. Mimi pamoja na wasichana tulijaribu kuwaza visingizio vya ghafla jinsi ambavyo tungeweza kumwambia bila kusema ukweli. Tulicheka sana tulipokuwa tunapanga visingizio vya ujinga wakati Gloria alipotuarifu kuwa Kocha alikuwa na binti mkubwa. Kuna uwezekano alikuwa ameanza kupata hedhi, kwa hivyo hapa kuwa na chochote cha kukionea aibu. Gloria alisema ukweli. Ingawa wanaume hawapati hedhi lakini wana mama, dada na wake ambao hupata, hivyo wanaelewa.

Hata hivyo, huku nikiwa na uoga na aibu kidogo, nilikwenda kwa Kocha na nikamwarifu kuwa nilikuwa kwenye siku zangu. Alichosema ni kuwa hakuna tatizo, angempigia mamangu ili aweze kuja kunichukua. Loo. Mazungumzo yalikuwa rahisi sana!

Siku iliyofuata niliamka nikihisi kama bingwa. Na kwa mtazamo huo nilijikaza na tukaweza kushinda mbio hizo! Nilipovuka mstari wa kumalizia mwanahabari alikuja ili kuwa na mahojiano na mimi.

“Hongera Kwassi! Unajihisi vipi?” akauliza.

Nikajibu, “Najihisi vizuri! Jana nilipatwa na hofu kidogo nilipoanza siku zangu, lakini niliamua kuwa sitokubali ziwe kizuizi. Nilijishughulisha tu na mbio na nafurahi sana kwa matokeo.”

Baada ya kufunguka kwa Kocha kuhusu siku zangu, sikuona haja ya kuaibika na chochote. Watu wengine hawaamini kwamba nilizungumza kuhusu siku zangu kwenye TV ya kitaifa lakini nani anajali! Hedhi ni kitu cha kawaida na hakuna chochote cha kuonea aibu kuhusiana nayo. Nafurahi pia timu yangu ilishinda!

Share your feedback