Zidhibiti chunusi zako!

Dondoo na mbinu rahisi

Maisha yamejawa kupanda na kushuka, na pale unapoanza Kubalehe unaweza kujisikia maisha kushuka zaidi ya yanavyopanda.

Mwili wako hupitia mabadiliko mengi sana katika kipindi cha kubalehe, vyote kihisia na kimaumbile. Ni vitu vingi unavyopaswa kukabiliananavyo, lakini ni vyema kutambua kile unachopaswa kukitarajia na kumbuka kuwa hii hutokea kwetu sote.

Wasichana huanza kuchomoza maziwa na kuanza kupata hedhi yao. Wavulana sauti zao huwa nzito na za juu. Nywele huanza kuota kwenye makwapa na katika sehemu za siri. Kutokana na mabadiliko haya ya homoni katika mfumo wako wa damu ni rahisi kujisikia mwenye hisia zenye kubadilika badilika na kupata chunusi.

Kiukweliii, chunusi huumiza- ni kana kwamba kila mtu anazitazama zilivyokubwa na nyekundu katika uso wako. Usiruhusu zikufanye ujisikie vibaya. Hazitodumu muda wote, na unaweza kufuata njia hizi za asili zitakazoweza kuisaidia ngozi yako...

1. Kunywa maji Mengi

Unywaji wa maji mengi unafaida nyingi sana. Asilimia 70 ya damu yako inatokana na maji, hivyo kunywa maji mengi kutasaidia mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula, na itakusadia kuondoa sumu mwilini na kuhakikisha mwili unapeleka virutubisho sahihi vinanyohitajika katika ngozi yako. Na matokeo yake ni kuwa na ngozi laini na inayong'ara.

2 Jaribu kupakaa mchanganyiko huu unaoponya

Mchanganyiko wa asali na mdalasini unapopakwa usoni husaidia kuondoa sumu kwenye ngozi yako. Vyote viwili vina sifa ya kuzuia miwasho na kuuwa bakteria. Changanya vijiko viwili vya asali na kijiko kimoja cha mdalasini ili upate mchanganyiko mzuri. Osha uso wako vizuri na Kisha upake mchanganyiko huu na uache ukae kwa Dakika 10-15 Kisha unawe. Fanya hivi Mara moja kwa wiki.

3. Punguza mawazo

Ni vigumu kuepuka kabisa msongo wa mawazo ( kazi za nyumbani, Wavulana, ndugu wakorofi,) lakini unaweza kukabiliana na msongo kwa kulala vizuri, kusali au kufanya mazoezi, au yoga, na kumbuka kupumua kwa nguvu kila Mara. Kadri unavyopunguza msongo wa mawazo ndivyo ngozi yako huonekana yenye afya zaidi.

Jaribu mbinu hizi rahisi na utajionea matokeo ya uhakika. Kama hakuna kinachoonekana kukusaidia, zungumze na mtu mzima unayemuamini ambaye anaweza kukushauri na kukuhakikishia kwamba hali hiyo haitadumu siku zote.

Oh na kumbuka... Kutokuwa na chunusi ama kuwa na chunusi hakubadilishi, wewe bado ni Mrembo!!

Share your feedback