Chunusi za hedhi

Je unakula vyakula vinavyokupa afya lakini bado wapata madoadoa?

Kula vyakula vinavyokupa afya kunaweza kukusaidia kuitunza ngozi yako, lakini kuna sababu zingine nyingi zaidi zinazoweza kuisaidia zaidi. Ukigundua unapata tatizo lile lile kila mwezi hili linaweza kutokana na homoni kutokuwa sawa.

Chunusi za hedhi husababishwa na mabadiliko katika homoni wakati wa mzunguko wako wa hedhi. Habari njema ni kwamba? Kujua mzunguko wako wa kila mwezi vizuri kunaweza kukusaidia kuepukana na chunusi.

Kabla ya hedhi: Mwili wako unatoa estrojeni na projesterone zaidi ili kusaidia kuandaa mwili wako kujiandaa kutoa yai. Hii huchochea tezi za mafuta, sehemu hii huwa na vijitundu vidogo vya kutolea jasho ambavyo vikiziba husababisha chunusi.

Wakati wa hedhi: testosteroni homoni huzalishwa kwa wingi wakati wa hedhi wakati huo huo homoni ya estrojeni kupungua. Katika wakati huu ngozi yako huweza kupata madhara kirahisi hivyo hakikisha unanawa uso wako na upake mafuta na jipende zaidi.

Baada ya hedhi: Huwa ni wakati wa madoadoa na chunusi kupungua. Ni kipindi ambacho mwili wako unarekebisha homoni zako na huwa ni kipindi kizuri sana kwa ngozi yako. Tabasamu – unastahili.

Wakati madoa yanapotokana na sababu zilizo ndani ya mwili hakikisha unaituza vizuri ngozi yako ili kutokuiharibu zaidi. Nawa uso na usipake mafuta mazito au vipodozi vyovyote vile unapokaribia hedhi.

Jambo la muhimu zaidi tambua kuwa watu wote wanaweza kupata madoa hasa wakati wa kubalehe, ni kipindi ambacho mwili wako unapitia mabadiliko mengi ya homoni. Hivyo usishangae kuona madoa katika ngozi yako. Kuwa mvumilivu upatapo chunusi zitokanazo na hedhi na usizitumbue zitaondoka zenyewe tu.

Ikiwa ngozi yako inakusababishia wasiwasi wowote mkubwa, zungumza na daktari kuhusu mbinu za kupambana na chunusi zako.

Share your feedback