Unajivunia hedhi au unaiogopa hedhi?

Wasichana wawili mapacha walikuwa na fikra tofauti kuhusu watakapovunja ungo!

Wakati Zena alipovunja ungo alifurahi sana. Alikuwa amesoma majarida mengi kuhusu hedhi na sasa ilikuwa ni wakati wake. Alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kumwambia pacha wake Amina.

Zena alipokwenda kumweleza Amina kuhusu hizi habari Amina alimjibu kwa sauti ya upole ‘’ooohh mimi pia nimevunja ungo’’ Zena alitabasamu na hakuelewa kwanini Amina hakuwa amemjulisha kuhusu hilo.

Zena alimshawishi dada yake kuketi na kuzungumza pamoja huku wakinywa chai.

Amina alihofia watamchukuliaje

Alidhani kila mtu angeweza kuona amebadilika, kilionekana ni kitu kikubwa sana kwake. Zena alimwambia kuwa hata yeyé alijisikia hivyo hivyo. Wasichana wote huvunja ungo, baadhi huwa inawatokea mapema zaidi na wengine huchelewa.

Amina alikiri alikuwa na hofu ya kuchafuka wakati damu inapotoka.

Zena alimwambia-ni kweli hilo linaweza kutokea lakini hata kama tukishindwa kupata pedi au tampons tunaweza kutumia vitambaa au kipande cha Kanga lakini tunapaswa kuhakikisha kuwa ni visafi. Huwa hatusikii aibu kuomba vitambaa vya kupengea makamasi hivyo hatupaswi kusikia aibu kuhusu jambo hili.– sisi sote tuna vitu sawa katika miili yetu!

Amina alikuwa anaona aibu kwani alidhani kuvunja ungo kulimaanisha amekuwa mwanamke na sio msichana tena.

Zena alimwambia huwezi kugeuka kuwa mwanamke ndani ya siku moja!. Aliendelea kumwambia kuwa huu ulikuwa mwanzo tu, lakini alikiri kuwa hata yeyé alijisikia kuhofia kukua na hata kuhusu maisha yake ya baadae. Walikumbushana michezo waliyokuwa wakicheza tangu walipokuwa watoto na waliahidiana kuendelea kuicheza kwa pamoja michezo hii ya kidada. Na wasingeweza kuiacha bila kujali umri wao.

Hatimaye Amina alikiri kitu kingine kinachompa hofu ni maumivu makali akiwa kwenye siku zake

Zena alimwelezea maumivu makali aliyopata hii ili msaidia Amina kutokuwa muoga. Aliona kama kila alichokuwa anakipitia Zena pia alikipitia. Walisoma zaidi kuhusu hedhi na waligundua kuwa maumivu wakati wa hedhi lilikuwa jambo la kawaida. Na walipata dondoo za jinsi ya kukabiliana na maumivu, kama vile kuwa vyakula vyenye afya, kufanya mazoezi kiasi, na kutumia chupa ya maji moto.

Share your feedback