Kubalehe kwaweza kuwa safari nyepesii

Usijisikie uko peke yako.

Miili yetu hubadilika sana wakati wa kubalehe, na wasichana wengi hujishangaa kama wao ni wa kawaida au la!. Mabadiliko haya yanaweza kuja na hisia za kuchanganya, lakini kuwa na uwezo ya kujifunza juu ya hisia hizo, na kuzungumza na marafiki wa karibu au familia, kunaweza fanya safari isiwe ya kukupa mawazo sana. Nilipoanza kubalehe, niliamua kumwambia shosti yangu kipenzi, ingawa mwanzoni nilijisikia aibu kidogo kuhusu hilo jambo. Kuzungumza kwetu kulitufanya tujiamini na kutokuwa wapweke.

Kubalehe huanza tunapokuwa na umri kati ya miaka 8-14. Wakati wa mabadiliko haya, mwili wako hutoa homoni kadhaa, na hizi huamsha ovari zetu kuanza kuzalisha estrojeni. Wakati mwingine mtiririko huu wa homoni hutufanya kupata hisia na kuchanganyikiwa. Hii ni ya kawaida kabisa, lakini cha muhimu kujua kwamba unaweza kuwaelezea hisia zako marafiki na watu wazima unao waamini. Watakusaidia kukupunguzia upweke, na wanaweza kukukumbatia au kukupa ushauri unapojisikia kuwa na huzuni. Ni kawaida kutojiamini wakati wa kubalehe. Mabadiliko mengi yanatokea, na wakati mwingine tunafikia hata kujilinganisha na marafiki zetu. Kumbuka kila mtu yuko katika safari yake mwenyewe, na tumeumbwa tofauti.

Kubalehe kwako kunapoanza, utapata mabadiliko machache ya mwili pia. Wakati mwingine mabadiliko haya ya kimwili yanaweza kukufanya uwe na hisia kali. Inaweza kuwa kitu cha ajabu kuona mwili wako ukibadilika na kutojisikia poa ni sehemu ya safari. Unaweza kuongezeka uzito, na kuna uwezekano mkubwa matiti yatakua pia na utaota nywele kwenye sehemu kama makwapani, miguuni, na hata sehemu za siri pia. Mabadiliko haya hutokea kwetu sote lakini yanaweza kuwa yenye hisia za ajabu mwanzoni. Ndiyo maana ni muhimu kuwa muwazi kuelezea hisia zako kwa marafiki zako. Kama una marafiki wa karibu wa kike basi utavuka kirahisi mno..

Kuomba msaada kunaweza kuogopesha wakati mwingine, lakini kuzungumza na shost yangu kuhusu kubalehe nilifanya jambo la maana. Tulipata nafasi ya kupeana uzoefu, na hii ilimaanisha kuwa kumbe nina mtu ambae naweza kuwa naye bega kwa bega.Kubalehe kunaweza kuwa ni safari rahisi, kama utapata msaada kwa watu wanaokupenda na kukujali.

Share your feedback