Je umewahi kusikia kuhusu maambukizi ya magonjwa ya zinaa?
Hivi unajua? Mimba sio hasara pekee ya kufanya ngono isiyo salama.
Unapofanya ngono bila kutumia kondom inakuweka katika hatari za kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Magonjwa ya zinaa yanasambazwa kwa kujamiiana.
Baadhi ya dalili za magonjwa haya ni kama vile:
Baadhi ya magonjwa ya zinaa huonyesha dalili mara tu unapoyapata na mengine huchukua muda mpaka dalili kuanza kuonekana - mfano ya magonjwa hayo ni kama vile Klamidia, kaswende na hata VVU. Pasipo kufahamu kama una maambukizi unaweza kujikuta unamuambukiza mwenza wako.
Magonjwa haya ya zinaa yasipotibiwa yanaweza kusababisha athari kubwa zaidi na kuumwa. Ndio maana ni muhimu sana kuufahamu mwili wako na kutambua unapokuwa sawa na mwenye afya. Mara tu unapojisikia kuwa tofauti nenda kafanyiwe uchunguzi haraka.
Jinsi ya kujilinda na magonjwa ya zinaa.
Matumizi sahihi ya kondomu ndio njia sahihi inayoweza kukulinda usipate magonjwa ya zinaa kwani sio njia zote za uzazi wa mpango zinaweza kukulinda dhidi ya magonjwa ya zinaa. Kwa mfano, ingawa vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kukukinga usipate mimba, lakini haviwezi kuzuia usipate maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Hivyo unapofikiria kuhusu njia za uzazi wa mpango kumbuka kuuliza kuhusu namna zinavyoweza kukulinda kwa namna mbalimbali. Ongea na mtu unayemwamini kama vile mama yako, shangazi au mtaalamu na mtoa huduma wa afya ili kujua zaidi.
Je upo katika mahusiano? Hii inakufaa zaidi !
Moja ya jambo muhimu sana kuhusu afya ya ngono ni namna wewe na mwenza wako mnavyozungumza. Wakati mnapokuwa tayari kuanza kufanya tendo la kujamiiana hakikisheni mnakuwa wawazi Kati yenu kuhusu historia yenu ya maswala ya ngono. Kama mwenza wako aliwahi kuumwa magonjwa ya zinaa unastahili kujua na kama wewe pia uliwahi kuumwa mwenza wako anastahili kufahamu.
Kabla hujaingia katika mahusiano yanayohusisha kujamiiana, Mara zote ni vyema muende wote katika kituo cha afya na mpime afya zenu. Njia hii itawasaidia kutambua kama mmoja wenu ana magonjwa ya zinaa au la!. Ni jambo zuri kuwa salama kuliko kuja kujuta baadaye.
Kama utahisi kuna uwezekano mkubwa kuwa unaweza ukawa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, hupaswi kamwe kuogopa. Nenda katika kituo cha afya au katika hospital na upime.
Kumbuka unafanya jambo la maana sana kutafuta msaada wa kidaktari na waala sio kitu cha kuonea aibu.Kwa kupata tiba sahihi magonjwa ya zinaa yanatibika.
Share your feedback