Ni kitu cha kawaida sana
Alama za michirizi ni jambo la kawaida kwa watoto wa kike na kiume wakati wa kubalehe.Unapoongezeka uzito kwa haraka (kama wakati wa kubalehe),unaweza kupata alama za mistari kwenye mwili wako. Hizo ndo alama za michirizi ya unene zilivyo.
Ikiwa unaona alama za michirizi kwenye mwili wako, hauko peke yako. Wasichana wengi na wanawake wanazo, sana sana kwenye matiti,mapaja,hipsi na makalio. Wanawake wengi huipata wakati wa ujauzito.
Alama za michirizi wala sio jambo la kulikuza kama baadhi ya watu wanavyochukulia. Ni sehemu tu ya ukuaji na ni kitu cha kawaida kwa watu wengi. Kumbuka, hakuna mwili wa mtu uliokamilika na kila mtu mwili wake ni wa pekee.
Uzuri halisi ni ule utokao ndani ya mtu, kwa hivyo hauhitaji kuwa na wasiwasi sana na muonekano wako wa nje. Ili uweze kukua, mwili wako lazima upitie mabadiliko fulani. Fikiria mtu wa umri wa miaka 30 awe mwili wa mtu wa umri wa miaka 10? hahahah si kituko!
Kubalehe ni safari ndefu.Sisi sote tuna changamoto zetu tunazopita, hivyo chukulia alama zako za michirizi kama vielelezo vya kila vita uliopigana na ukashinda. Au sio jamani?
Alama za michirizi huwa zinafifia kadri unavyozidi kuendelea kukua, lakini kuna baadhi ya mambo unaweza kufanya ili kuzidhibiti wakati unapobalehe.
Tumia mafuta ya asili ya mwili kama ya nazi au ya cocoa kutoka kampuni ya shea ambayo huwa yana vitamini E. Yanasaidia sana kufanya ngozi iwe nyororo and kupunguza makunyanzi.
Kunywa maji kwa wingi ili kuongeza maji mwilini. Itazuia uwezekano wa ngozi kutokuwa na mikunjo.
Fanya mazoezi mara kwa mara na kula chakula chenye virutubisho. Kwa njia hiyo utaweza kudhibiti uzito wako. Kujinyoosha mara kwa mara pia hufanya ngozi yako kuwa laini na hupunguza Kuonekana kwa alama za mistari ya michirizi.
Kumbuka; usiruhusu mwonekano wako wa nje kuathiri hisia zako za ndani.Uzuri wako ni zaidi ya huo muonekano wako, hivyo zingatia mambo ambayo ni muhimu!
Share your feedback