Pedi

Utahitaji moja kati ya hizi, siku kadhaa kila mwezi!

Labda umekiona kwenye mfuko wa dada yako au mama yako na ukashangaa ni cha nini. Basi, inaitwa pedi!

Wakati utawadia ambapo mwili wako utapitia mabadiliko. Hii inaitwa ubalehe na hii inakuja na kuanza kwa kupata hedhi. Tunatumia pedi wakati wa hedhi. Kabla ya kupitia jinsi ya kuvitumia tuanze na kinachofanyika wakati wa hedhi.

Kupata hedhi ni sehemu ni kile tunachoita mzunguko wa mwezi, jambo linalotokea kila mwezi kutayarisha miili yetu kupata mimba. Inatokea hivi:

Day_1-7.png

1). Siku 1-7: mzunguko wa hedhi huanza ambapo, ukuta ndani ya tumbo lako la uzazi huondoa ukuta wake wa ndani uliobomoka kupitia uke wako. Hii inaitwa hedhi na inatokea kwa siku kadhaa, kulingana na kila mwanamke. Hapa ndipo tunatumia pedi kunyonya ile damu.

Day_7-14.png

2). Siku 7-14: Hapa ndipo wakati wa kukomazwa yai hufanyika. Ovari zako hujitayarisha kukomaza yai. Kwa wakati huu, tumbo lako la uzazi pia huanza kujiandaa kulipokea yai kwa kutengeneza ukuta mpya.

Day_14-17.png

3). Siku 14-17: Hapa, ovari zako zinaachilia lile yai na linaenda hadi kwenye tumbo lako la uzazi. Huu ni wakati ambapo unaweza kushika mimba haraka sana. Tumia njia za uzazi wa mpango unapofanya ngono kama hauko tayari kupata mimba - na kujikinga na magonjwa ya zinaa.

Day_17-25.png

4). Siku 17-25: Yai huendelea kusafiri katika tumbo la uzazi. Kama halitatungishwa, litavunjika na kutolewa nje ya mwili.

Day_25.png

5). Siku ya 25: Mwili wako utatoa ukuta wa ndani wa tumbo lako la uzazi kama ute uliochanganyika na damu (hedhi yakon) na mzunguko wa hedhi utaanza upya.

Maajabu? Hivyo ndivyo hedhi huwa. Hata hivyo sio mzunguko wa hedhi wa kila mtu utafuata muundo huu. mizunguko ya hedhi hubadilikabadilika,na hicho ni kitu cha kawaida.

Sasa tunajua Pedi ni za kazi gani. Hivi ni baadhi ya vidokezo unapotumia Pedi:

New_napkin.png

a). Hakikisha Pedi ni mpya na imefungwa, ili kuhakikisha ni salama na safi.

Remove_strips.png

b). Toa ile sehemu ya plastiki ya pedi kabla ya kuiweka juu ya chupi yako, ili kutumia gundi iliyo nyuma yake. Gundi ile huweka Pedi salama kwenye chupi yako. Lasivyo inaweza kudondoka.

c). Kuna pedi za aina kadhaa, kulingana na bajeti yako na mahitaji. Chagua inayokutosha vizuri.

Change_napkin.png

d). Badilisha pedi inapojaa au baada ya masaa sita. Itupe vizuri ili uwe safi kila wakati!

Share your feedback