Ndege na nyuki

Usiwe na aibu, hata maua yanatakiwa kuzaliana!

Mada ya ngono ni pana sana- ni pana sana huwezi ukamaliza kuichambua kupitia makala moja - hivyo tunaivunja katika sehemu ndogo ndogo. Hebu tuanzie mwanzo kabisa, hiki ni nini hasa na kwanini watu wanapenda kuifanya.?

Ni kwa kupitia ngono ndipo binadamu na wanyama huweza kuzaliana, na hii ni sehemu ya maisha. Vitazame vipepeo. Ni kana kwamba wanafurahia kuruka ruka wakizunguka katika bustani, lakini husaidia uchavushaji, kwa kuweka poleni katika maua, ili tuweze kuwa na maua mengi zaidi duniani. Je hili sio jambo la kufurahisha?

Tunapokuwa bado wadogo, akili na miili yetu huwa bado havikomaa kuanza kuzaliana. Lakini wakati huwa unafika na wote tunapevuka na kuwa tayari kuanza kuzaliana. Hiki kipindi ndio kile tunakiita "kubalehe". Ni katika kipindi hiki ndipo mwili huipitia mabadiliko mengi sana ya kimaumbile na kihomoni. Kwa wasichana, hubalehe wakiwa na miaka Kati ya 10 na 14. ( kwa wavulana wao huchelewa kidogo na hubalehe wakiwa na miaka Kati ya 12 na 16)

Kwa wasichana, kubalehe kunamaanisha pia utaanza kupata hedhi. Mara tu msichana anapovunja ungo tayari mwili wake unakuwa na uwezo wa kubeba mimba. Hata hivyo, ni vyema mtu kuhakikisha kwamba yupo tayari kifikra na anaweza kumudu majukumu ya kuwa na mtoto.

Wakati wa ubalehe, wengi wetu huanza kuwaona watu wanaotunzunguka kwa namna tofauti. Unaweza ukawa unampenda mtu fulani hivi sasa, mtu ambayo huwezi kuacha kumfikiria muda wote, Je jambo hili linakufanya ujisikie kuchanganyikiwa? Usijali! Ni jambo la kawaida kuvutiwa na mtu, na linaweza kuwa jambo lenye kuvutia mno.

Pamoja na mabadiliko mengi yanayotokea katika mwili wako, pamoja na mawazo na hisia nyingi unazozipata, na hata inapokuja katika swala la mapenzi, unaweza kuhisi Kuchanganyikiwa na unaweza kuwa na maswali mengi. Hata kuhusu ngono. Ni muhimu kupata taarifa sahihi kutoka kwa mtu unayemwamini, hivyo pole pole, utaanza kufurahia. Kuuelewa mwili wako ni mwanzo kujielewa na kujipenda!

Share your feedback