Jamani nini kimeutokea mwili wangu?

Kubalehe... Kila mtu huipitia hatua hii!

Inawezekana umeshuhudia na kujisikia tofauti siku za hivi karibuni, baadhi ya sehemu katika mwili wako zinabadilika na imekuwa rahisi kukasirika kwa haraka. Haya yote ni mambo ya kawaida- huku kunamaanisha kubalehe.

Kubalehe? Hebu nieleze zaidi...

Kila mmoja wetu yupo tofauti ila moja ya vitu ambavyo tunafanana wote wavulana kwa wasichana ni kile tunachokipitia kipindi cha kubalehe. Hiki ni kipindi katika maisha yako ambapo inaonyesha sasa unaelekea utu uzima. Unaweza kubalehe mapema sana Kati ya umri wa miaka 7 au 8 na kipindi hiki huendelea kwa miaka Kati ya minne au mitano, lakini haijalishi lini utaanza kubalehe, watu wote hupitia kipindi hiki.

Muda wa mabadiliko

Vitu vingi vitaanza kutokea mwilini kwako yakiwemo yafuatayo:.

  • Matiti yako yatakuwa
  • Utarefuka zaidi
  • Nywele na ngozi yako vitakuwa na mafuta zaidi
  • Mwili wako utaongezeka na umbo lako litakuwa zaidi.
  • Unaweza kuanza kupata chunusi
  • Utaota nywele makwapani na kwenye sehemu zako za siri
  • Utavunja ungo(Hedhi)

Kila unachotakiwa kukifahamu kuhusu hedhi yako

Unapofikia kipindi cha kubalehe moja ya Kati ya maj badiliko muhimu sana katika mwili wa msichana ni pale unapovunja ungo.

Katika hatua za awali za hedhi yako, homoni zako hufanya mayai katika ovari zako kukomaa. Hatua itakayofuata, ovari zako zitaruhusu mayai kutolewa. Wakati huo huo homoni zako zitausaidia mwili kutengeneza ukuta ndani ya tumbo lako la uzazi, ili kama yai au mayai yako yatarutubishwa na mbegu za kiume kwa njia ya kujamiiana, ukuta uwe tayari kupokea mimba.

Kama mayai hayatarutubishwa, ukuta huu huondolewa kama kimiminika chenye mchakanyiko wa damu (hedhi). Hivi ndivyo ilivyo walaa! hakuna kitu cha ajabu ama chakutisha, ni kwamba mwili wako unafanya mambo yake.

Kubalehe inaweza kuonekana kama kitu cha kuogopesha , lakini kumbuka kwamba watu wote hupitia hatua hii, hivyo tambua haupo peke yako Binti.

Share your feedback