Mwili wako unajiweka sawa!
Huenda unashangaa kwanini hedhi yako huwa unaona inachelewa na kuwahi miezi mingine na wakati mwingine isije kabisa.Miezi ya mwanzo ya hedhi huwa hakuna siku maalumu ya kuingia kwenye siku zako,na hiki kitu cha kawaida sana.
Mwili wako unakuwa unajifunza kuweka sawa mizunguko yako ya mwezi na hii inaweza kuchukua miezi au hata miaka kabla haijakaa sawa.
Kuna sababu nyingine zinazofanya mzunguko wako usiwe na mpangilio maalumu na hii inaweza kuwa u mwembamba sana,mnene sana,mwenye mawazo mengi au kutokuwa na madini chuma ya kutosha mwilini.
Ikiwa hedhi yako haiji kabisa, hii inaonesha mwili wako unakupa meseji flani.Kutunza afya ni muhimu,kwa hiyo hakikisha unakula vyakula vilivyo na protini (kama kuku, mayai na karanga) na upate usingizi wa kutosha.
Njia bora ya kufuatilia hedhi yako ni kuhesabu mzunguko wako, ili uweze kujua ni lini utaingia kwenye siku zako.Ikiwa ni mzunguko wa siku 28, hedhi yako inapaswa kudumu siku 5 hadi 7.Hivyo hesabu kutoka siku ya mwisho uliyomaliza hedhi kwa mwezi uliopita hadi siku kwanza ya hedhi inayofuata.Fanya hivi kwa miezi mitatu na kama idadi ya siku kati ya kumaliza na kuanza hedhi ni tofauti sana kila mwezi,basi hii ina ina maana mzunguko wako hauna mpangilio maalumu.
Baadhi ya wasichana hawana uwiano mzuri wa homoni unaosababishwa mtindo wa maisha (mazoezi mengi au kujipunguza mwili kwa lishe, msongo wa mawazo au kutumia vidonge vya uzazi wa mpango) au tatizo la kiafya (kama polycystic ovarian syndrome).
Ni muhimu kuanza kuutunza mwili wako. Kujithamini mwenyewe kutakusaidia kupunguza msongo wa mawazo,mazoezi ya kutosha yatakufanya uwe imara na kuzalisha homoni za kujisikia vizuri,na ulaji bora wa kiafya utakuhakikishia mwili wako unapata nguvu inayohitaji kufanya kazi vizuri.
Ikiwa hutapata hedhi yako kwa miezi michache au ikiwa itachukua muda mrefu zaidi ya siku 7, basi unashauriwa kwenda kumwona daktari wako au zungumza na mtu mzima ambaye unaemuamini na unajisikia poa kuongea nae.
Share your feedback